Akizungumza
leo,Mganga Mfawidhi hospital ya wilaya ya Kahama Dkr,Charles Rwaikeza,alisema kuwa
jumla ya watoto kumi na nane wamezaliwa usiku wa mkesha wa sikuku ya Christmas wote wakiwa wamezaliwa salaama bila matatizo yoyote.

Dr.Rwaikeza alisema kuwa alipokea takwimu za
watoto waliozaliwa kutoka kwa wakunga waliokuwa zamu ambapo ilikuwa jumla ya
watoto kumi nane wamezaliwa wakiwa na afya njema sambamba na wazazi waliojifungua watoto hao wakiwa na siha njema.
Hata hivyo Rwaikeza aliwataka
wakina mama waepuke kujifungulia nyumbani badala yake pindi wanapojihisi
mabadiliko ya kimwili wakati wa ujauzito wawahi katika hospital ama zahati
zilizo karibu nao ili kupata matibabu ikiwa ni njia mojawapo ya kujifungua
salaama.
Aliongeza kuwa pindi wakina mama
wajawazito wanapokuwa hospitalini wakisubiri wakati wa kujifungua na kupata
usumbufu kutoka kwa wauguzi wasisite kufika katika ofsi ya mganga mfawidhi kwa
lengo la kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yanayokuwa yamejitokeza kwa wauguzi wa
zamu.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI