Thursday, December 25, 2014

ASKOFU ATAKA AMANI ILINDWE

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

 ASKOFU Ludovick Minde wa kanisa katoliki
jimbo la Kahama, amewaasa Watanzania  kuhakikisha tunailinda na kuienzi Kwa vitendo amani iliyopo nchini sambamba na kutatua changamoto zinazojitokeza ambazo zinazoweza kuvuruga upendo , umoja na mshikamano wa taifa letu.


Akihubiri katika misa takatifu ya krismasi iliyofanyika

katika kanisa kuu la jimbo la Kahama , Askofu Minde alisema Wakristo duniani wanaposherekea
kuzaliwa kwa Bwana Yesu kristu,wanapaswa iwajenge zaidi katika amani, upendo , utulivu , mshikamano
na ushirikiano katika taifa letu.


Askofu Minde alisema amani
iliyopo isiwe ya kauli za mdomoni,bali jamii inapaswa
kuzitatua changamoto hizo kivitendo zinazoweza kuhatarisha , upendo, umoja ,
mshikamano wa taifa letu na kuendelea kumuomba Mungu aendelee kuijalia  tunu
hiyo.


Akizungumzia juu ya changamoto za maisha katika familia, alisema
kila wanafamilia wanawajibika kuzitatua vizuri bila kuathiri upendo na mapenzi mema kwa watu anaoishi nao.

 “Ndugu zangu waumini sikukuu hii ya krismasi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu ambayo ni sherehe ya kusherekea kwa pamoja na
familia,lazima kuachana na matendo mabaya yote ikiwemo ubinafsi, chuki, wivu , mifarakano kwa kumuomba Mungu ajalie
amani , upendo popote pale hata kama ni makazini.”Aliwaasa Askofu Minde.

Aidha akitoa salamu za krismasi kwa waumini wa jimbo la Kahama baada
ya misa , Askofu Minde aliwatakia  sikukuu jema ya kuzaliwa kwa Yesu kristu , upendo na mafanikio katika maisha na familia zetu na kuwataka kuendelea kumuomba Mungu aendelee kujaalia amani na mshikamano.









 

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI