Saturday, December 27, 2014

WANANCHI WASHIRIKIANE NA VIONGOZI KULETA MAENDELEO

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

WANANCHI wa mtaa wa Igalilimi Kata ya Kahama mjini wilayani Kahama
mkoani Shinyanga wametakiwa kuondoa makundi yaliyokuwepo wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na badala yake waoneshe ushirikiano na viongozi waliochaguliwa ili kufikia maendeleo waliotarajia kwa wakati.

Mwenyekiti wa Mtaa huo Ibrahim Khan  alisema hayo na kuomba juhudi zilizooneshwa kwa umoja baina ya wananchi na viongozi wa vyama wakati wa kampeni za uchaguzi zitakakiwa
kuhamishiwa katika kupigania maendeleo kwa kuwaunga mkono viongozi waliochaguliwa bila kujali itikadi ya vyama vyao.

Alisema kama wananchi wataunganisha nguvu kwa kuonesha ushirikiano itasaidia mtaa huo kusonga mbele kwa haraka kimaendeleo katika maeneo yote.
Katika hatua nyingine Khan aliwashukuru wananchi wa mtaa huo kwa kumchagua kuwa mwenyekiti ambapo ameahidi kuwa kwa kushirikiana na wajumbe wake watahakikisha wanafanya kazi bila ya kuwepo kwa upendeleo wowote.

Aidha alisema atahakikisha wanaboresha miundombinu hususani maeneo korofi ambapo kwa kushirikana na halmashauri ya Mji na serikali wilayani humo watahakikisha wanafanikisha kuboresha maeneo hayo.

Uchaguzi wa serikali za Mitaa hufanyika kila baada ya miaka mitano ambapo mwaka huu imefanyika disemba 14 licha ya kuwepo kwa dosari kadhaa ambazo zilifanya baadhi ya maeneo kusogeza mbele kwa uchaguzi huo.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI