Zikiwa zimebaki siku
chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, ofisi ya waziri
mkuu TAMISEMI imetangaza jumla ta watanzania 11,491,661
wamejiandikisha na wanatarajiwa kupiga kura.
Idadi hiyo ambayo ni
sawa
na asilimia 62 ya matarajio ya watu 18,587,742 ambao walitarajiwa
kuandikishwa kama asilimia 42 ya watanzania wote kwa mujibu wa sensa ya watu na
makazi ya mwaka 2012.
Takwimu hizo zimetolewa
na mkurugenzi wa uchaguzi wa serikali za mitaa Khalist Luanda wakati
akizungumzia hali ya uchaguzi huo na maandalizi yake kwa ujumla hapa nchini.
Luanda amesema hadi leo
maandalizi ya uchaguzi huo yalikuwa yakiendelea na kulikuwa na hali nzuri kwa
maeneo yote nchini.
Mkurugenzi huyo amesema
tayari halmashauri zote zimeshachapisha majina ya wagombea pamoja na nembo za
halmashauri zao ambazo ndizo zitakazotumika kwa maeneo yote.
Kwa upande mwingine
ameutangaza mkoa wa Katavi kuwa umeibuka kinara kwa kuandikisha wapiga kura kwa
asilmia 79 ukifuatiwa na Kagera ambao uliandikisha kwa asilimia 78, wakati
wilaya za Mpanda na Babati zikifanya vizuri kwa kati ya asilimia 107 (mpanda)
na 101 kwa babati.
Mikoa iliyofanya vibaya ni Dar es salaam ambao uliandikisha
kwa asilimia 43 na Kilimanjaro kwa asilimia 50 wakati wilaya zilizofanya vibaya
ni Kilindi mkoani Tanga (21%) na wilaya ya Same-Kilimanjaro iliandikisha
kwa 22%.
Amesema kuwa TAMISEMI haijawa na takwimu sahihi za wagombea
waliokuwa wameshindwa kuendelea na uchaguzi baada ya kuwekewa mapingamizi na
kwamba bado wanafuatilia ili kujua wangapi wamewekewa mapingamizi hayo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI