Friday, December 12, 2014

JAMII ISHIRIKIANE NA POLISI KUTOKOMEZA UKATIRI WA KIJINSIA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



KAMANDA wa Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan ameitaka jamii kushirikiana na kitengo cha dawati la jinsia na watoto kutoa elimu ili kuyatomeza matendo ya ukatili wa kijinsia.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa

kinjsia , Shekhan amesema jeshi la polisi kupitia kitengo hicho limekuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii kujiepusha na matendo hayo maovu dhidi ya jamii. .

Amesema kila mmoja kwa nafasi aliyonayo , anapaswa kuwajibika kuufikisha ujumbe kwa jamii ili iweze kujilinda na matendo hayo ambayo yamekuwa yakitshamiri siku hadi siku.

Katika madhimisho hayo ambayo yameenda sambamba na zoezi la usafi wa mazingira pamoja na kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa hospitalini hapo , kamanda shekhan amewataka akinamama kuwa mstari wa mbele zaidi kupinga matendo hayo.

Kwa upande wake muuguzi wa wodi ya watoto katika hospitali hiyo, sabra salim Suleiman, amelipongeza jeshi la polisi kutokana na mchango wake katika kusafisha mazingira ya hospitali hiyo .

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI