WATU
kumi ambao ni wafuasi wa chama cha mapinduzi, katika kata ya kalangalala
Wilayani Geita,wamenusurika kuchomwa moto na wananchi wakati wakigawa chumvi
ili kuwashawishi wananchi kuchagua viongozi wa chama hicho katika uchaguzi ujao
wa serikali za mitaa.
Katika
tukio hilo,vigogo wa CCM mkoa akiwemo mbunge wa viti maalumu Vicky Kamata,
walifika eneo la tukio kwa lengo la kuwakingia kifua watuhumiwa hali
iliyopelekea polisi kutishia kuondoka eneo hilo ili wananchi wajitawale.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia desemba 10,2014 saa 3.30 usiku na kulilazimu
jeshi la polisi kutumia nguvu ya ziada kuwashawishi wananchi kutojichukulia
sheria mkononi kwa kuwapiga na kuwachoma watu hao mbele ya vyombo vya dola.
Kufuatia
zoezi hilo la ugawaji wa chumvi baadhi ya wananchi waliwapigia simu wanahabari
ili kushuhudia tukio hilo na kwamba watuhumiwa hao walikuwa ndani ya nyumba ya
balozi wa chama hicho wakati wa ugawaji huo.
Kufuatia
ghasia hizo polisi waliwataka vigogo hao wa CCM kuwa wapole huku wakitishia
kuondoka eneo hilo ili wananchi wafanye watakavyo kutokana na vigogo hao kutaka
kutumia vyeo vyao kuwafundisha kazi askari polisi.
Aidha
wanachama hao walifikishwa kituo cha polisi Wilaya ya Geita wakiwa na pakiti
zao za chumvi ambazo walikuwa wakizigawa kwa wananchi.
Kwa
mujibu wa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Geita John Maro,
watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na upelelezi
ukikamilika watafikishwa mahakamani.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI