BAADA ya kucheza mechi saba katika nusu ya kwanza ya Mzunguko wa Kwanza wa Ligi kuu ya soka ya Tanzania bara,huku ikishinda mechi moja na nyingine sita wakitoka sare,hali iliyoashiria kuna maradhi yanayoisakama timu kongwe ya Simba Sport Club,sasa gonjwa hilo limekomaa kiasi cha kukubali kipigo cha bao 1 - 0 dhidi ya Kagera Sugar.
![]() |
Simon Serunkuma akifanya vitu vyake. |
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam baada ya
mapumziko ya mwezi mmoja na nusu wakati ligi hiyo iliposimama,Klabu hiyo kongwe iliyofanya usajili wa gharama kwa kusajili wachezaji watatu raia wa Uganda hivyo kuweka rekodi ya kuwa na wachezaji watano wote kutoka nchi moja,hadi mapumziko wana wa Msimbazi walikuwa nyuma kwa bao hilo.
Bao hilo pekee lilifungwa kwenye dakika ya 21 na mshambuliaji wa
zamani wa Yanga na Coastal Union Atupele Green ambaye alifanyia kazi
makosa ya kipa wa Simba Ivo Mapunda na beki Mohamed Hussein .
Kwa matokeo haya Kagera Sugar wamefikisha pointi kumi na tatu baada ya michezo nane na wanapanda mpaka kwenye nafasi ya nne .
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI