HATIMAYE Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama imekamilisha
uchaguzi wake uliokuwa umekwama huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo “CHADEMA”
kikiuletea mtikisiko mkubwa Chama Cha Mapinduzi “CCM”kwa kutetea viti vyake na
kupata vingine vilivyokuwa
katika himaya ya CCM.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
hiyo,Patrick Karangwa,alisema Uchaguzi huo umemalizika kwa amani na
utulivu ingawa kuna vitongoji vitatu mshindi ameshindwa kupatikana baada ya
kura kulingana
Karangwa alisema CCM imeshinda kwa kupata nafasi
73 za vijiji kati ya 92 vilivyopo katika Halmashauri hiyo ya Msalala huku chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kikipata nafasi 19 za vijiji.
Aidha Karangwa alisema katika Halmashauri yake
kuna Jumla ya vitongoji 390 ambapo CCM kimepata nafasi 299 huku CHADEMA
wakipata 84 na UDP viwili pamoja na Chama Cha wananchi CUF kikipata kiti kimoja
Uchaguzi huo wa viongozi wa serikali za mitaa Jumapili
iliyopita ulishindwa kufanyika ambapo mkurugenzi huyo alisema ni kutokana na
sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa kiutendaji
Sababu zingine zilizoelezwa na Karangwa
kukwamisha uchaguzi huo ni pamoja na umbali wa eneo la kiutawala na makao makuu
ya Halmashauri hiyo ambapo siku hiyo magari ya kusambaza vifaa yalishindwa
kufika kwa wakati kwenye vituo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kuharibu
barabara.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya
Msalala,Emmanuel Bombeda alisema chama chake na washirika wake wa vyama vya UDP
na CUF,wamekiletea mtikisiko mkubwa chama tawala kutokana na idadi ya viti
walivyotwaa ambavyo ni mataji mkubwa kwa uchaguzi mkuu ujao.
“Hadi tunaenda kwenye uchaguzi wa Serikali za
mitaa,tulikuwa na viti viwili tu ambavyo ni kuwa na Serikali ya Kijiji cha
Kakola na Ilogi ambavyo tumevitetea na kuongeza vijiji vingine 17 vilivyokuwa
chini ya CCM,na kwa upande wa vitongoji hatukuwanacho hata kimoja leo kwa
ujumla wetu tunavyo 87,kwetu ni ushindi mkubwa,”alisema Bombeda.
Msalala
ni moja ya Halmashauri tatu zinazounda wilaya ya Kahama ambazo mbali na hiyo
pia zipo zingine mbili za Ushetu na mji wa Kahama ambazo Jumapili iliyopita
zilifanya uchaguzi wake wa viongozi wa serikali za mitaa
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI