WAKAZI wa Bukondamoyo katika
Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wameingiwa na hofu baada ya
bibi kizee mmoja kudaiwa kudondoka kwenye
ungo akidaiwa kutoka mkoani Tabora kusherekea sikukuu ya Chrismas
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio
hilo lililokusanya umati mkubwa wa watu wamedai bibi kizee huyo alidondoka alfajiri
huku akidai alikuwa na wenzie watano ambao walifanikiwa kutoroka kuelekea kijiji
cha Ndugu kata ya Kinaga wilayani Kahama
Aidha bibi kizee huyo baada ya
kuhojiwa na hili gazeti tando alisema anaitwa Chausiku huku akidai
alikuwa akielekea katika kijiji hicho cha ndugu
Hata hivyo jeshi la polisi wilayani Kahama
liliwahi kufika kwenye tukio na kumuokoa bibi kizee huyo ambaye alionekana
kuvaa nguo zilizochakaa na makovu katika mkono wake wa kushoto ambapo imedaiwa
alichubuka wakati akidondoka
Tukio hilo limehusishwa na imani za
kishirikina kwa kuwa ungo ni kifaa kinachoaminiwa kutumika kwa nguvu ya giza
kupaa angani kama usafiri unaotumiwa na wanga katika shughuli zao za nguvu ya
giza ikiwemo uchawi
Na Shija Felician - Kahama.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI