Mzunguko wa Kwanza.
Katika pambano hilo lililkuwa la kuvutiwa huku ufundi wa wachezaji hao ukionyeshwa zaidi na viungo wa timu hizo hadi timu zinaenda mapumziko zilikuwa zimefungana bao 1 - 1,ambapo wana lambalamba walitangulia kupata bao mnamo dakika ya 5,kwa bao lililofungwa na Mshambuliaji wa zamani wa Yanga,Didier Kavumbagu baada ya mabeki wa Yanga kuchanganya na kipa wao Deogratias Munishi "Dida".
Yanga ilijipatia bao la kusawazisha mnamo dakika ya 7,na Mshambuliaji aliyetemwa dakika za mwisho na mahasimu wao,Hamis Tambwe,aliyewahi kwa kichwa krosi ya Salum Telela,na kupachika mpira kimiani,na kuamsha shangwe za mashabiki wa Wana Jangwani.
Mnamo dakika ya 52 ya mchezo,Simon Msuva aliipatia timu yake bao la pili baada ya kufunga kwa kichwa mpira mrefu uliopigwa na Haruna Niyonzima,lakini dakika ya 65 mpira wa kwanza kwa John Bocco "Adebayor"aliyeingia badala ya Salum Abubakari, unamuwezesha kufunga bao kwa kichwa kutokana na krosi safi ya Himid Mao.
HUKO Mbeya,Timu ya Mbeya City baada ya kuboronga katika mechi saba za mwanzo za Ligi Kuu Bara, kimezinduka na kupata ushindi,ikiwa nyumbani katika uwanja wa Sokoine, kwa kuifunga Ndanda FC kwa bao 1-0.
Vijana hao wa Mbeya City walijipatia Bao hilo la ushindi mapema katika dakika ya 3 tu,kwa bao maridadi lililofungwa na Deus Kaseke,ndilo lililodumu hadi mwisho wa mchezo.
KATIKA Uwanja wa Manungu Complex,Mtibwa Sugar ilifanikiwa kupata sare katika Uwanja wake huo wa nyumbani baada ya kusawazisha dakika kumi za mwisho wa mchezo dhidi ya Stand United,iliyopata bao la mapema.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya kiporo baada ya
kuahirishwa jana kutokana na mvua kubwa kusababisha maji kujaa uwanjani.
Kutokana na hali hiyo, mechi hiyo ilianza
kuchezwa kuanzia dakika ya sita ambayo iliishia jana.
Na katika mchezo uliochezwa Jana Usiku katika uwanja wa Azam Complex,
Chamazi, Dar Ruvu JKT walifanikiwa kuibuka kwa ushindi wa bao 1 - 0 dhidi ya ndugu zao wa Ruvu Shooting.
Nayo Polisi Morogoro iliibuka kwa ushindi wa bao 2 - 0,yaliyopachikwa kimiani na Nicholas Kabipe na Imani Mapunda. KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI