SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, idadi ya watu
waliofariki duniani kutokana na mfumuko wa ugonjwa wa homa ya Ebola huko
Magharibi mwa Afrika imeongezeka na kufikia 5,147 huku watu
wengine 14,068
wakiambukizwa ugonjwa huo.
WHO imeongeza kuwa, vifo vingine 13 na watu 30 wameambukiwa
katika nchi 5 za Nigeria, Senegal, Mali, Uhispania na Marekani.
Shirika hilo limeongeza kuwa, maambukizo ya ugomjwa huo
yamepungua katika nchi za Guinea na Liberia lakini yameendelea kuongezeka huko
Sierra Leone ambako kumeripotiwa kesi mpya 421 za maambukizi katika wiki moja
hadi kufikia Novemba 9.
Wataalamu wa afya walisema, idadi ya kesi mpya ni muhimu sana
kuliko wanaokufa kutoka na ugonjwa huo, kwani inaakisi jinsi virusi vya Ebola
vinavyosambaa.
Watu wasiopungua 75 waliwekwa katantini katika mji mkuu wa
Mali, Bamako baada ya kufariki dunia muuguzi mmoja aliyekuwa na ugonjwa huo.
Wakati
huo huo shirika la Madaktari wasio na mipaka, MSF limesema litafanya majaribio
ya tiba mpya ya Ebola katika vituo vitatu Afrika Magharibi.
Wafanyakazi hao
watatumia dawa aina mbili zilizoainishwa na Shirika la Afya duniani, WHO.
Sababu ya
kufanyika kwa majaribio hayo ni kuwafanya Wagonjwa kuendelea kuwa hai wakati wa
siku 14 za mwanzo tangu maambukizi ya ugonjwa huo.
CHANZO cha Habari ni Tehran swahili &BBC
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI