![]() |
Mwanamke mwenye umri wa miaka 60
aliyekatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe
anayefahamika kwa jina moja la Mashaka. |
WITO umetolewa kwa wananchi
kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahalifu pindi
vinapotokea vitendo vinavyoashiria
uvunjifu wa amani.Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo baya, mama huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete ambapo anadaiwa kukutwa na kisanga hicho hivi karibuni.
Mwanamke
huyo anadai kujeruhiwa na mumewe usiku wakati wakiwa wamelala nyumbani
kwao Mtaa wa Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora.
Akizungumza
na mwanahabari wetu kwa tabu akiwa wodini kwenye hospitali hiyo akiwa
na maumivu makali, mama huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Siku
ya tukio, nakumbuka mume wangu alikwenda kutembea, aliporejea nyumbani
alifuatana na mtu mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji.
“Walipofika
nyumbani aliniambia yupo na mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akitafuta
viungo vya sehemu za siri za mwanamke akiwa na fedha milioni tano.
“Mimi
nilikataa baada ya kunishawishi lakini usiku nilipokuwa nimelala, mume
wangu alinikata huku akiniamuru nisipige kelele kwa kuwa alikuwa
ameshapatana bei na kwamba ulikuwa ni utajiri mkubwa.”
Alisema baada ya tukio hilo alijikuta amelazwa hospitalini hapo hivyo hajui kama mumewe huyo alishakamatwa au la.
Kwa
mujibu wa majirani zao, Mtaa wa Kazaroho, lilikuwa ni tukio la kutisha
kwani wasamaria wema ndiyo waliomkimbiza mama huyo hospitalini ili
kuokoa uhai wake.
Majirani
hao walimtaka Waziri wa Maendeleo ya Wanawake Jinsia na Watoto, Sophia
Simba kufanya kazi ya ziada ili sheria ichukue mkondo wake ili
kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyoshamiri
kwa kasi nchini.
Kwa
mujibu wa mmoja wa madaktari hospitalini hapo ambaye hakutaka kutajwa
jina kwa kuwa si msemaji, mama huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa
katika hali mbaya lakini baadaye alipata nafuu hivyo anaendelea vizuri
na matibabu.
Jitihada
za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Suzane Kaganda
aliyehamishiwa mkoani hapa hivi karibuni hazikuzaa matunda hivyo
zinaendelea. via>>Jamvi la Habari.com
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI