WAONGOZA watalii nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa
wanasaini mikataba halali ya kazi na wamiliki wa makampuni wanayofanyia kazi
ili kuepuka kunyonywa haki zao.
Rai hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na
Utaliii, Mahmoud Mgimwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha waongoza
watalii mlima Kilimanjaro kilichofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema, hifadhi ya mlima Kilimanjaro ndiyo hifadhi
inaingizia serikali mapato makubwa ikilinganishwa na hifadhi nyingine, hivyo
kuwataka waongoza watalii kufanya kazi kwa umakini kwani kutofanya hivyo
watalikosesha taifa mapato yatokanayo na utalii katika mlima huo.
Aliwaahidi waongoza watalii hao kuwa, atakutana na
chama cha wamiliki wa makapuni ya utalii nchini pamoja na chama cha
wamiliki wa makampuni ya utalii Kilimanjaro ili kuona namna ya kulinda maslahi
ya waongoza watalii.
Kwa upande wake mkuu wa
hifadhi ya KINAPA, Erasto Lufungulo, alisema waongoza watalii wamekuwa
sehemu kubwa katika kuyatunza mazingira ya hifadhi ya mlima huo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI