WANANCHI wa Kijiji cha Kanegere kata ya
Bukandwe Wilaya Mbogwe Mkoani Geita wameiomba Serikali kuingilia kati kupinga
kitendo cha Mwekezaji kuwapatia wananchi Notisi ya kuhama kijijini hapo
ili kupisha shughuli za utafiti wa madini kijijin hapo.
Wakiongea na Wandishi wa Habari, Wananchi
hao walisema kitendo kilichofanywa na mwekezaji huyo sio cha
kiungwana kwani
kaya zilizopo Kijijini humo zipo kwa muda mrefu na kuwaondoa bila kufuata
sheria ni kukiuka haki za kibinaadamu.
Walisema Mtafiti huyo yupo tangu
muda mrefu na haieleweki anatafiti nini na hata katika shughuli za kijamii
amekuwa akikwepa kuchangia katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika
kijiji hicho zaidi ya kuwafukuza wachimbaji wadogo wanaochimba dhahabu.
Mmoja wa Wachimbaji hao Zacharia Maghembe
alisema Mwekezaji huyo yupo katika eneo hilo kwa miaka 22 ambapo anachokifanya
ni kubadilisha makumpuni ya utafiti na kuzuia shughuli za mendeleo katika
kijiji hicho akidai maeneo hayo ni yake.
Akijibu tuhumza hizo Meneja utafiti
wa Kampuni ya Mabangu Mining Limited William Harmsworth amekiri kwa kuwafukuza
wachimbaji hao katika maeneo hayo ili kupisha ujenzi wa mgodi huo.
Harmsworth alisema Kampuni hiyo inawataka
wananchi wote katika Kijiji hicho kuhama mapema iwezekanavyo kupisha ujenzi wa
Mgodi unatarajiwa kuanza wakati wowote katika eneo hilo huku kukiwa hakuna
ushahidi wa mwekezaji huyo kuwa na leseni ya uchimbaji.
Alisema Mabangu Mining Limited itafanya
upembuzi yakinifu katika eneo hilo ili kumlipa kila Mwananchi anayeishi
katika Kijiji hicho kulingana na eneo lake na thamani ya nyumba anayoishi ili
kupisha shughuli za uchimbaji kabla ya kuanza.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI