EMMANUEL Okwi akongoza wenzake kushangilia bao. |
Alikuwa ni
Mshambuliaji wake
Raia wa Uganda Emmanuel Okwi ambaye alicheza mchezo wake wa
nne ilhali akiwa mgonjwa ndio aliyeivua klabu yake koti lenye mzimu wa sare kwa
kuipachikia bao mnamo dakika ya 79,kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.
Okwi anaifungia Simba bao baada ya kuumiliki
mpira mbele ya mabeki wa Ruvu Shooting na kutoa pasi kwa Maguri aliyepiga shuti
kali, kipa Shooting Abdallah Rashid akatema na Okwi akamalizia wavuni.
Baada ya bao hilo Okwi alikimbilia
kushangalia katika jukwaa la Yanga ambapo mashabiki wa watani hao muda wote wa
mchezo walikuwa wakimzomea kwenda kuwaziba mdomo ambao nao walimrushia chupa za
maji.
Ushindi huo wa kwanza katika Ligi kwa
msimu huu pia na kwa uongozi wa Rais Aveva umeifanya timu hiyo kufikisha pointi
Tisa baada ya kutoka suluhu mechi sita.
Katika
pambano hilo lilionyesha dhahiri Simba kuibuka na ushindi kutokana na kucheza
mchezo wenye malengo lakini kikwazo kilikuwa maafande hao ambao walionyesha
umakini mkubwa katika kudhibiti mashambulizi ya Simba iliyopata kona Tisa huku
Shooting ikiwa haijapata hata moja.
MASHABIKI wa Simba wakishangilia ushindi wao wa kwanza. |
Baada
ya Dakika 90 za mchezo kocha wa Simba Patrick Phiri akiwa mwenye furaha alidai
ushindi huo unatokana na kikosi chake kuimarika sikua hadi siku,huku kocha wa
maafande wa Ruvu Shooting, Tom Olaba akisema timu yake ilicheza vizuri
isipokuwa haikutumia vyema nafasi ilizopata.
Nazo
timu za Mtibwa Sugar na Kagera Sugar, zilihitimisha kiporo chao cha pili kwa kutoka sare ya bao
1-1.
Ikumbukwe
katika mchezo wa siku ya Jumamosi ambao ulivunjika wakati Mtibwa Sugar
ikiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Ame Ali.
Lakini
mvua kubwa ikalazimu pambano liahirishwe na leo asubuhi kwenye uwanja wa
Manungu, dakika 45 zilizobaki zikamaliziwa.
Kagera
ikapata bao lake kusawazisha kupitia kwa Rashidi Mandawa katika dakika ya 57.
Sare
hiyo ni ya tatu kwa Mtibwa Sugar ambayo imeshinda mara nne na kuendelea kubaki
kileleni.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI