WAKULIMA
wa zao la pamba wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kufuata sheria kumi
za uzalishaji wa zao hilo ili kupata pamba itakayokuwa na ubora zaidi.
Meneja wa kampuni ya ununuzi na uchambuaji wa
pamba (KCCL) Bahati Bayala alisema wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi
kutokana na wakulima kutokuwa na uelewa juu ya kilimo cha pamba hasa kutozingatia
kanuni la zao hilo.
Alisema
kuwa serikali inalo jukumu la kuwaelimisha wakulima wa zao hilo kupitia Mabwana
Shamba ambao ndio walengwa watakaoweza kuwapatia elimu wakulima wa zao hilo juu
ya uandaaji pamoja na uvunaji.
Kwa upande
wake Meneja wa kampuni ya NIDA Gregory Kabuta alisema iwapo wakulima wa zao
hilo watazingatia kanuni za kilimo bora za pamba ikiwa ni pamoja na kutumia
mbolea za samadi kutasaidia kupata pamba yenye ubora zaidi.
Kabuta alisema
suala la ugawaji wa mbegu wamezigawa katika maeneo mbalimbali huku
wakiwahamasisha wakulima kujiaandaa na msimu wa mwaka 2014 na 2015.
Aliwataka wakulima kuzingatia utunzaji wa mashamba, na
kuwakumbusha wakulima kutochanganya maji na mchanga kwenye pamba kwa
lengo la kuzidisha kilo hali ambayo inapunguza ubora wa zao la pamba.