BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO
 |
NAIBU Waziri wa Uchukuzi Dkt.Charles John Tizeba akiongea.
SERIKALI imedhamiria kukomesha vitendo
vya wizi wa vifaa mbalimbali vya magari bandarini kwa kuandaa mkakati maalumu utakaosaidia
kutambua wahusika wafanyao vitendo hivyo vinavyolitia doa Taifa.
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa
Uchukuzi Dkt.Charles John Tizeba ambapo alibainisha kuwa serikali imeweka
dhamira ya dhati kutokomeza vitendo hivyo ambavyo kwa kipindi kirefu vimekuwa
vikilalamikiwa na watu wanaoagiza na kusafirisha magari yao kwa njia ya maji.
|
|
|
Dkt.Tizeba alisema imekuwa kawaida watu wengi kulalamikia vitendo
vya wizi wa vifaa mbalimbali katika magari eneo la bandari ya Dar es Salaam, hatua
ambayo imesababisha Serikali kutoa tamko rasmi juu ya mkakati unaoandaliwa ili
kukomesha wizi huo.
Akizungumzia juu ya kukabiliana na
vitendo vya wizi wa vifaa vya magari bandarini Naibu Waziri huyo alisema pamoja
na kwamba jitihada zilizokwishafanyika zimepunguza uhalifu huo lakini lengo ni
kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa kabisa.
 |
Dkt.Tizeba akisisitiza jambo kwa uongozi wa Wizara,Bandari na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo cha Kupakia na Kupakua Makontena TICTS;Neville Bisett.
Alifafanua katika mkakati ulioandaliwa
ni kuwepo kwa mfumo unaoendana na teknolojia ya kisasa ambayo itakayohakikisha
inatambua kasoro zilizo kwenye gari kabla halijatolewa katika meli.
Aidha alisema baada ya kufahamu kasoro
hiyo,pia mfumo huo utaendelea kubaini mapungufu mengine baada ya gari hilo
kushushwa toka katika meli na siku ya kuchukuliwa na mmiliki mwenyewe hivyo
kama itaonekana na kasoro na kubainika tatizo hilo lilijitokeza kipindi gani na
wapi.
|
|
Alisema kupitia mkakati huo hakuna
udanganyifu na uhalifu utakaofanyika pasipo wahusika kubainika hali ambayo
itasaidia kukomesha matukio hayo ya wizi wa vipuri vya magari hasa kwakuwa
wahalifu wake watapatikana na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Kumekuwa na vitendo vya wizi
unaosababisha upungufu wa vipuri vya magari yanayoagizwa kutoka ng’ambo jambo
ambalo limekuwa likipigiwa kelele na wadau mbalimbali wanaoagiza magari
ughaibuni.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI