Friday, November 14, 2014

KIFUSI CHAUA WANAFUNZI WAKIFANYA KAZI YA MWALIMU

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


 





 

JESHI la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Ilomba wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kwa tuhuma za kusababisha vifo vya wanafunzi watatu baada
ya kuwatumikisha katika kazi zake binafsi katika maeneo na mazingira hatarishi.

Kamanda Polisi mkoani Mbeya,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi "SACP"Ahmed Msangi,alisema Mwalimu huyo Isambi Mwasenga{57},alitumia madaraka yake kuwaita na kuwatumikisha katika shughuli za uchimbaji vifusi wanafunzi watatu wa kike wanaosoma darasa la nne katika shule hiyo.

. Alisema wanafunzi hao walipatwa na mauti hayo baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba udongo ndani ya shimo kwa lengo la kuupeleka kwa mwalimu huyo aliyewaagiza kumfanyia kazi hiyo,ndipo wakati wakichimba udongo ndani ya shimo walifukiwa na kifusi cha udongo kilichokuwa sababu ya vifo vyao.

Kamanda Msangi alisema tukio hilo lilitokea Novemba 12,mwaka huu majira ya saa sita mchana na kuwataja wanafunzi waliofikwa na umauti huo kuwa ni Sevelina Mwile[11], Mkazi wa Kitongoji cha  Itale, Grace Pastson[10],Mkazi wa Kitongoji cha Itale na Agey Seme [10],Mkazi wa Kitongoji cha Ilomba wilaya ya Mbeya vijijini.

Alisema awali kabla ya kukutwa na mauti hayo,wahanga hao walichukuliwa shuleni na Mwalimu huyo kwenda kumfanyia kazi binafsi ya kuchimba udongo na kumpelekea nyumbani kwake,ndipo walipofikwa na maafa hayo.

Miili ya Marehemu ilikabidhiwa kwa ndugu tayari kwa mazishi baada ya kufnyiwa uchunguzi wa kitabibu,huku mtuhumiwa akiendelea kuwa mahabusu wakati Upelelezi wa Shauri lake ukiendelea na taratibu zikikamilika atafikishwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

 
Aidha Kamanda Msangi alitoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kuwatumikisha kazi watoto wenye umri mdogo katika maeneo na mazingira hatarishi yatakayowza kusababisha kusababisha maafa huku akisisitiza kufanya vitendo vya namna hiyo ni kwenda kinyume cha sheria

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI