IMEBAINIKA kuwa wanafunzi
wa kike 53 nchini Kenya wanaofanya mitihani ya kumaliza Kidato cha nne ni
wajawazito.
Kubainika huko
kumekuja kutokana na taarifa iliyotolewa na Afisa Elimu katika Kaunti ya
Bungoma Kenya,iliyotaja idadi
hiyo ya wanafunzi wanaofanya mitihani ya kuhitimu
elimu ya sekondari iliyoanza siku ya Jumanne wiki hii ni Wajawazito.
Katika taarifa
yake Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti hiyo;Charles Anyika iliyochapishwa na News
24 Kenya,imesema huenda idadi hiyo ikawa ni ndogo.
Taarifa hiyo
ilibainisha kuwa uchunguzi uliofanyika katika eneo dogo umefaulu kutambua hali
hiyo,ambapo inategemea kwa mazingira halisi na ukubwa wa eneo la nchi hiyo
idadi ya wanafunzi wenye ujauzito inaweza kuwa kubwa zaidi.
Ufafanuzi ulieleza
kuwa inategemea kuwa idadi ya idadi ya wanafunzi wenye ujauzito ikawa ni kubwa
kuliko iliyopatikana kwa kuwa baadhi ya wakuu wa shule walitoa taarifa za uongo
na pia baadhi ya familia wamekuwa ‘wakimalizana’ na watuhumiwa bila ya kutoa
taarifa.
Anyika alisema
awali kabla ya uchunguzi huo walitegemea idadi ya wanafunzi wenye mimba kufikia
100, wakati huo huo amewataka walimu wawaache wanafunzi hao wafanye mitihani
yao kwa utulivu na kuwaagiza walimu kuandaa magari ambayo yatasaidia iwapo
mwanafunzi yoyote atapata dharura.
Aidha
aliwataja walimu, waendesha ‘bodaboda’, na wanaume waliooa ni wahusika wa mimba
hizo na kuongeza kuwa umaskini ni chanzo kikubwa cha tatizo hilo, na kuwataka
wazazi kuwalinda watoto wao na kuwapa elimu juu ya hatari ya mimba za utotoni
pamoja na ngono zembe.