WAKATI Serikali ya
Nigeria ikihaha kuwapata na kuwarejesha kwa wazazi na walezi wao wasichana
waliotekwa
na Wapiganaji wa Boko Haram,kikundi hicho cha wapiganaji kimefanya
mashambulizi na kufanikiwa kufanya utekaji mwingine mkubwa wa binadamu.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyoripotiwa na Shirika la la Utangazaji Uingereza “BBC” imeeleza kwamba
kikundi cha wapiganaji cha Boko Haram kimefanya mashambulizi katika kijiji cha
Adamawa kilichopo Kaskazini Magharibi ya Nigeria na kuteka wanawake na
wasichana katika kijiji hicho.
Boko Haram
waliahidi kuwaachilia huru zaidi ya wasichana 200 wanaoshikiliwa na kikundi
hicho,lakini badala ya kutekeleza ahadi hiyo,wamefanya utekaji wa wasichana na
wanawake hao ikiwa ni siku sita tangu serikali ya Nigeria na kikundi hicho
walipofanya makubaliano hayo.
Hata hivyo japo
Boko Haram wamekiuka makubaliano waliyoafikiana Ijumaa iliyopita, bado serikali
ya Nigeria ina matumaini ya kuachiliwa huru kwa wasichana hao baada ya kikao
kinachotarajiwa kufanyika muda wowote kuanzia sasa huko Chad.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI