UGONJWA wa Ebola
umeendelea kuwa tishio kwa nchi za Ukanda wa Magharibi ya Afrika baada ya nchi
ya Mali kuthibitisha kupatikana kwa mgonjwa wa kwanza wa maradhi hayo.
Serikali ya Mali
imethibitisha kuhusiana na taarifa za mtoto wa miaka 2 kukutwa na maambukizi ya
Ebola akiwa ni mtu wa kwanza kupata maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo tangu
ugonjwa huo ulipozuka mwezi Machi 2014.
Kwa mujibu wa Taarifa
kutoka mtandao wa THE WORLD POST zimesema, mtoto huyo amegundulika kuwa na
maambukizi ya ugonjwa huo aliporejea nchini humo akitokea Guinea, moja ya nchi
zilizoathiriwa zaidi na Ebola Afrika Magharibi.
Mali inakuwa nchi
ya sita kutangaza kupatikana mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola katika ukanda
wa Afrika Magharibi, lakini ndani ya siku 7 nchi za Senegal na Nigeria
zimetangaza kutokuwa na mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola.
Ripoti iliyotolewa
na WHO imeonesha vifo zaidi ya 4,900 vimetokea katika nchi za Sierra Leone,
Guinea na Liberia.
Timu ya
wanasayansi wa kimataifa imejipanga kutafiti uwezekano wa kutumia damu ya mtu
aliyewahi kupona Ebola kama tiba ya ugonjwa huo.
Mali inapakana na
nchi ya Guinea kwa upande wa Kusini Magharibi, lakini mtoto huyo anakuwa
mgonjwa wa kwanza kuripotiwa kuwa na maambukizi ya Ebola nchini humo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI