SHULE ya Sekondari ya Anderlek Ridges iliyo katika Halmashauri ya Mji
wa Kahama imetumia kiasi cha Shilingi Milioni 83,500,000/= kupanda jumla ya
miti 9356 katika eneo la Shule ili
kuhakikisha inatunza vyema mazingira ya
shule na kufanikisha kutoa na kupata elimu bora kwa vijana watakaobahatika
kusoma shuleni hapo.KIONGOZI wa mbio za Mwenge Kitaifa 2014,Rachel Stephen Kassandaakizindua Klabu ya Malihai inayojihusisha na utunzaji mazingira katika Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges. |
KIONGOZI wa mbio za Mwenge Kitaifa 2014,Rachel Stephen Kassandaakipanda Mti shule ya Sekondari Anderlek Ridges. |
Kwa mujibu wa Taarifa iliyosomwa mbele ya kiongozi wa Mbio za Mwenge
Kitaifa kwa mwaka 2014,Rachel Stephen Kassanda na katibu wa Klabu ya Mazingira
shuleni hapo Onesmo Nicholus,alisema katika idadi ya miti hiyo,miti 3400
waliipanda baina ya mwaka 2012 hadi 2014.
Nicholaus alisema Klabu ya Mazingira Shuleni hapo ilianzishwa mwaka
2010 ikiwa na wanachama 30 wakiwa ni wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha
nne na kwa sasa ina wanachama 54 wakiwa katika uwiano sawa baina ya wavulana na
wasichana,ambapo amajukumu yao makubwa mbali na masomo ni kuratibu na kusimamia
utunzaji wa mazingira ya shule ili kuwa bora kwa kutoa na kupata elimu.
Alisema Klabu hiyo pia inajihusisha na kuelimisha jamii kuhusu athari
za moto na namna ya kukabiliana nazo,kutoa elimu ya mabadiriko ya tabia
nchi,elimu ambayo wanaipata hapo shuleni na kuahidi kuiendeleza hata mara baada
ya kuondoka katika familia ya shule hiyo.
MKURUGENZI wa Shule ya Sekondari ya Anderlek,Mr.Alexander Kazmil akipokea kikombe cha Tuzo ya Rais Mazingira,kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2014,Rachel Kassanda. |
“Tunafurahi kupata bahati ya kujifunza kwa vitendo na kushiriki katika
shughuli za utunzaji wa mazingira na upandaji miti,tunaahidi kuendeleza jitihada
hizi za utunzaji mazingira na upandaji miti popote pale duniani mara baada ya
masomo yetu”,alise Nicholaus.
VIJANA wa Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges wakiwa katika mstari huku wakiimba kwa furaha wakati wa mapokezi ya Mwenge. |
Aidha kwa upande wake Kiongozi wa Mbio zza Mwenge Kitaifa kwa mwaka
2014,Rachel Stephen Kassanda aliupongeza uongozi wa shule hiyo kuonyesha
unafundisha kwa vitendo mambo muhimu yenye ustawi kwa Taifa kama utunzaji wa
mazingira na upandaji miti.
KIONGOZI wa mbio za Mwenge Kitaifa 2014,Rachel Stephen Kassanda akikagua vifaa vya kuhifadhia taka. |
Kassanda alisema elimu wanayopata na kushiriki kwa vitendo kwa
wanafunzi katika utunzaji wa mazingira itakuwa msaada mkubwa kuondokana na
uharibifu wa mazingira katika jamii ya Watanzania hivyo kutoa wito kwa shule
zote nchini kuhakikisha zinaanzisha klabu za mazingira hatua itakayosaidia
kulirejesha taifa katika uoto wa kijani.
Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges imefanikiwa kutwaa Tuzo ya Rais
ya Usafi na Utunzaji Mazingira kwa mwaka 2013/2014 kwa shule za sekondari nchini
baada ya kushika nafasi ya kwanza Tanzania bara na kupatiwa Cheti na hundi ya
ShilingiMilioni Tatu.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI