BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO
 |
WANAFUNZI wanaobaki wa Shule ya Msingi na Awali Agape Lutheran ya wilayani Kahama wakionyesha umahiri wao kucheza ngoma za utamaduni. |
SIKU moja mara baada ya Bunge
maalumu la katiba kuwakabidhi viongozi wakuu wa nchi Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Serikali ya Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Sheini katiba pendekezwa,Kanisa
la
KKKT wilayani Kahama limeibuka na
kuwataka wanasiasa kuacha tabia ya
kuwabeza na
kuwakejeli viongozi wa dini.
 |
MWALIMU Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi na awali Agape Lutheran ya wilayani Kahama,Pamela Vuluwa akimakabidhi Risala ya Shule,Mgeni rasmi katika mahafari ya wahitimu wa darasa la saba na la awali kwa mwaka 2014,Diwani wa Kata ya Kahama,Abasi Omary. |
Kauli
hiyo ilitolewa juzi na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
Dayosisi kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Jimbo la Kusini Magharibi KKKT Usharika wa Agape Kahama,Daniel Mono wakati wa mahafari ya
tatu kwa shule ya Msingi Agape na ya kumi na nne kwa darasa la awali la shule hiyo.
 |
MWALIMU Mkuu katika Shule ya Msingi na awali ya Agape Lutheran,Paschal Masanja,akisoma risala ya shule,aliyeshaika Kipaza Sauti ni Mwalimu Mkuu Msaidizi Pamela Vuluwa. |
 |
DIWANI wa Kata ya Kahama Abasi Omary akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Shule ya Msingi |
Mchungaji
Mono alitumia fursa hiyo hiyo kuwakemea wanasiasa
hao kufuatia kauli iliyotolewa hivi karibuni kabla ya kuvunjwa kwa Bunge
Maalumu la Katiba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo Samweli Sitta
kuwashambaulia baadhi ya viongozi wa dini kwa kuita waraka waliotoa
katika makanisa wakitaka vikao vya bunge Maalumu visitishwe ili kuokoa
fedha za wananchi kuwa ni wa kipuuzi.
 |
DIWANI wa Kata ya Kahama,Abasi Omary akiongea na Wahitimu,Wanafunzi,Walimu na Wazazi katika Mahafari ya Shule ya Msingi na Awali ya Agape Lutheran ya mjini Kahama,kushoto kwake ni Askofu Emmanuel Makala na kulia kwake ni Mchungaji Daniel Mono. |
 |
WAHITIMU wa elimu ya Msingi wenye suti,walijikuta wakiingia kuserebuka katika onesho la ngoma na wanafunzi wanaobaki. |
 |
DIWANI wa Kata ya Kahama katika Halmashauri ya Mji wa Kahama,Abasi Omary akitoa cheti cha uongozi bora kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi na Awali ya Agape Lutheran,Paschal Masanja,anaeshuhudia akitabasamu mwenye suti ni Askofu Emmanuel Makala. |
 |
DIWANI wa Kata ya Kahama,Abasi Omary akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa darasa la awali katika shule ya Msingi na awali ya Agape Lutheran ya mjini Kahama. |
Mchungaji
huyo alidai wana siasa wamekuwa na tabia ya kutumia majukwaa yao
kuwashambulia kwa
lugha chafu viongozi wa dini pindi wanapokemewa kutokana na kufanya
vitendo kwa maslahi yao binafsi,paspo kujali kashfa wazitoazo kwa
viongozi wa dini zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani hasa kutokana na
viongozi hao wa kidini kuwa na kundi kubwa la waumini linalowaamini.
 |
ASKOFU Emmanuel Makala akiongea katika Mhafari. |
Aidha
Askofu wa kanisa hilo Emmanuel Makala alisema viongozi wa dini wanatambua uwepo
wa serikali ambayo huwekwa madarakani na Mungu lakini tatizo lililopo kwa sasa
ni upatikanaji wa viongozi waliolelewa katika maadili ya dini na kuona umhimu
wao wa kuwatumikia wananchi.
 |
WANAFUNZI wanaoaki wakionesha umahiri wao wa kucheza muziki wa Kizazi kipya |
 |
WANAFUNZI wanaobaki wakiimba Kwaya. |
Askofu
Makala alisema ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi unaofanyika nchini
kwa hivi sasa ni matokeo ya viongozi wa kisiasa kukosa uzalendo
kunakotokana na kutolelewa kwa kupata mafunzo na maadili ya kidini hivyo
kuiomba jamii kuhakikisha vijana wao wanapatiwa mafunzo ya kiroho ili
kujakupata viongozi waadirifu na wazalendo wa nchi.
 |
MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi ya Ziwa Victoria Usharika wa Agape Kahama,Mchungaji Daniel Mono akiongea. |
 |
MENEJA wa Shule,Clement Telugwa |
Kabla
ya hapo Menejaa wa Shule hiyo Clement Telugwa alisema shule hiyo ambayo
inamilikiwa na Kanisa hilo la KKKT ina wanafunzi 302 na ina mchepuo wa
Kiingereza ambayo inafundisha wanafunzi wote pasipo kujali itikadi za
kidini.
 |
KATIKA Mahafari hayo zilikuwepo burudani mbalimbali ikiwemo Kwaya hii |
Telugwa alisema hali hiyo inaimarisha umoja na
mshikamano katika jamii kwakuwa suala la elimu
la kila Mtanzania hivyo kutokana na hali hiyo shule hiyo pamoja na kuwa
inamilikiwa na taasisi ya dini inazingatia Umoja wa kitaifa.
 |
WAHITIMU wa elimu ya Msingi na awali |
Naye
Diwani wa Kata ya Kahama Abasi Omary kabla ya kukabidhi vyeti hivyo kwa wahitimu
46 kwa shule ya Msingi na awali 19 aliwataka wazazi kuitumia shule hiyo bila
kuangalia msimamo wa kidini.
Diwani huyo alisema watoto hao wanaokwenda shuleni hapo ni
kuajili ya kupata elimu na si kubadili dini hali ambayo aliwataka wazazi
kuzingatia hilo kwakuwa elimu inayotolewa katika eneo hilo ni muhmu kwa kizazi
kilichopo kwa maslahi ya Taifa.
 |
WANAFUNZI wanaobaki wakionesha umahiri wao katika kuimba na kucheza |
Pamoja na hali hiyo Mkuu wa Shule hiyo Paschal Masanja
alisema Shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa uzio na mabweni hali inayosababisha
kuwa na usalama mdogo wa uhifadhi wa mali zake na utunzaji wa
Mazingira.
Hata
hivyo Masanja alisema uongozi wa kanisa hilo umeanza mkakati wa ujenzi wa uzio
utakaogharimu Shilingi Milioni 25,pamoja na mabweni mawili ya kuanzia
yatakayogharimu Shilingi Milioni 78,fedha hizo ni kutoka kwa waumini na wadau
mbalimbali wa elimu.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI