Monday, October 6, 2014

MWENGE ULIPOINGIA MKOANI SHINYANGA NA KUSHUHUDIA MIRADI 41 KAHAMA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

WANAFUNZI  vijijini walijitokeza kuushuhudia Mwenge.
MWENGE wa Uhuru ulipokelewa kutoka mkoa wa Geita katika kijiji cha Mwabomba Kata ya Idahina,Halmashauri ya Ushetu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga,na kuona na kuzindua miradi 41 yenye thamani ya
Shilingi Bilioni 6 katika wilaya ya Kahama ambayo ina Halmashauri tatu za Ushetu,Mji na Msalala.

BWANA huyu na mwanae alihakikisha anaushika Mwenge

Katika mkesha wa mapokezi ya Mwenge kijiji cha Mwabomba Kata ya Idahina,Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama ambapo ndipo Mwenge ulianza kukimbizwa,watu 168 kati yake wanaume 147 walijitokeza kupima kwa hiari ambapo waliopatikana na maambukizi ni 13 ambapo kati yake mwanamke alikuwa mmoja.

 KATIKA mapokezi ya Mwenge kulikuwa na shamrashamra nyingi zikiwemo ngoma za asili,kama hii ya kuchezea majoka.




KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI