![]() |
SIMON Msuva akimtoka beki wa Prison |
YANGA
SC imezinduka na kupata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara baada ya kuilaza
Prisons ya Mbeya mabao 2-1 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Mnamo dakika ya 34 ya mchezo alikuwa mchezaaji wa kulipwa wa timu hiyo Andrey Coutinho,raia wa Brazil alipoipatia Yanga SC bao la kuongoza kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa zaidi ya mita 25, baada ya Mrisho Ngassa kuangushwa.
Katika kipindi hicho cha kwanza mshambuliaji tegemeo kwa sasa wa Yanga SC, Mbrazil, Genilson Santana Santos ‘Jaja’ alishindwa kuipatia timu yake mabao zaidi kutokana na kushindwa kutumia vizuri nafasi mbili nzuri alizotengenezewa mnamo dakika ya 31 na 42.
![]() |
ANDREY Coutinho akishangilia bao alilofunga. |
Vijana
wa Jangwani wanaofundishwa na Mbrazil Marcio Maximo, ilicheza vizuri kipindi
cha kwanza, pamoja na Prisons kuonyesha
upinzani, lakini dhahiri ilizidiwa na kuonyesha kuwa baada ya Yanga kupoteza
mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mtibwa sasa imezinduka.
Wajelajela hao
timu ya Prisons kutoka Mbeya ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa pungufu, baada
ya beki wake, Jacob Mwakalobo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 39 baada ya
kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na refa Andrew Shamba wa Pwani, kufuatia
kumchezea vibaya Ngassa.
Kipindi
cha pili, Prisons walibadlika na kuanza kusukuma mashambulizi yenye uhai
langoni mwa Yanga SC- hali ambayo iliwafanya wapate bao la kusawazisha dakika
ya 67, mfungaji Ibrahim Kahaka aliyetokea benchi ambaye alimalizia pasi ya
Jeremiah Juma.
![]() |
RAHA ya ushindi |
Lakini
bao hilo halikudumu, kwani dakika mbili baadaye, Simon Msuva aliifungia Yanga
SC bao la ushindi akimalizia krosi maridadi ya Ngassa kutoka upande wa kulia.
Baada ya hapo, timu hizo zilianza kushambuliana kwa zamu na Prisons walilalamika kunyimwa penalty baada ya beki na Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuunawa mpira kwenye boksi.
Kikosi
cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Edrwad Charles, Kevin
Yondan/Rajab Zahir dk77, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Haruna
Niyonzima, Hassan Dilunga/Hamisi Thabit dk54, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho
Ngassa na Andrey Coutinho/Simon Msuva dk58.
Prisons;
Mohamed Omar, Salum Lameya, Laurian Mpalile/Boniface Hau dk74, Nurdin Chona,
Lugano Mwangama, Jumanne Elfadhil, Meshack Olest/Julius Kwangwa dk35, Freddy
Dungu, Jacob Mwakalobo, Amin Omary/Ibrahim Kahaka dk53 na Jeremiah Juma.
Aidha
katika pambano linguine lililochezwa katika dimba la Azam Complex timu ya
Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa bao 2 – 1 dhidi ya maafande wa JKT Ruvu.