Sunday, September 28, 2014

SIMBA HAIJAPONA GONJWA LAKE,YALAZIMISHWA SARE.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

EMANUEL Okwi akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao




GONJWA lililokuwa likiwasibu Vijana wa Wekundu wa Msimabazi “Simba Sports Club”msimu uliopita bado
halijapatiwa tiba msimu huu,baada ya mara ya pili mfululizo kushindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani,kwa kulazimishwa sare ya bao 1 – 1 na maafande wa Polisi Moro.

 KIPA Abdul Ibad akichupa bila mafanikio kuokoa shuti lililozaa goli la kwanza,lililofungwa na Emmanuel Okwi.
Katika dakika ya 32 , Emmanuel Okwi aliifungia Simba bao la kuongoza akimalizia pasi ndefu ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kutoka upande wa  kushoto wa uwanja, huku mabeki wawili wa Polisi akiwemo Lulanga Mapunda wakimuacha Mganda  huyo atulize mpira kifuani katika eneo la hatari na kutikisa nyavu.
MSHAMBULIAJI Dan Mrwanda wa Polisi Moro akipongezwa na wenzake baada ya kuisawazishia timu yake bao.
Mnamo dakika 50 Danny David Mrwanda alifunga goli la kusawazisha baada ya mabeki wawili wa Simba, Masoud Nassor ‘Cholo’ na nahodha Joseph Owino kugongana na kumuacha nyota huyo wa zamani wa Simba akifunga.
Kabla ya mechi hiyo, Septemba 20 mwaka huu, Mnyama aliambulia sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu uwanja huo huo wa Taifa.







Simba walianza mechi kwa kutawala safu ya kiungo ambapo Jonas Mkude alionesha kiwango kizuri. Alitawala dimba la kati, alikuwa na jeuri, alipiga pasi sahihi na kuipandisha timu juu, lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili.
Mkude alionekana kuchoka, wakati huo huo Piere Kwizera, Shaaban Kisiga, Emmanuel Okwi waliokuwa mbele yake walishindwa kurudi nyuma ipasavyo na kuisaidia timu.

Aidha katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar Es Salaam bao mbili zilizowekwa kimiani kila kipindi na Didier Kavumbagu yaliiwezesha timu ya Azam kuibuka na ushindi wa bao 2 – 0 dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting.
Nao vijana wa Stendi United kutoka mkoani Shinyanga walizinduka usingizini baada ya kuifunga Mgambo JKT katika uwanja wa Mkwakwani Tanga kwa bao 1 – 0.Na kwenye uwanja wa Manungu Turiani Morogoro Mtibwa waliendeleza wimbi la ushindi kwa kuibabajua Ndanda FC kwa bao 3 – 1.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI