MWANDISHI wa habari kutoka Kahama FM Bakari Khalid akiwasilisha majibu yaliyotokana hoja iliyotolewa na Mwezeshaji Emma Mashobe.
WANAUME wilayani Kahama katika mkoa wa Shinyanga wameaswa kubadilika katika mtazamo chanya juu ya malezi ndani ya familia zao ili kuweza
kuondokana na mfumodume unaowakandamiza
wanawake na watoto hali ambayo imeonyesha
kuwepo kwa ongezeko la ndoa za
utotoni.
|
MWANDISHI wa habari wa magazeti ya Mwananchi,Mwanaspoti na The Citizen Mkoani Shinyanga Shija Felician,akichangia mada katika semina ya siku tatu inayotolewa na Care International wanaotekeleza Mradi wa Wanaume na Wavulana katika kuleta Mabadiriko ya Kijinsia. |
Hayo yalielezwa na Meneja wa mradi wa Wanaume na Wavulana katika kuleta Mabadiriko ya Kijinsia "Men-engage" Emma
Mashobe kutoka shirika lisilo la kiserikali la Care- International katika semina ya siku tatu inayoshirikisha waandishi wa habari 15 kutoka Mkoani Shinyanga inayofanyika mjini Kahama.
Wandishi wa Habari wakimsikiliza mwezeshaji katika mafunzo hayo
Mashobe alisema mradi huo ulioanza mwaka 2012 unatarajia kufikia ukomo Desemba mwaka huu ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kupata mawakala wa mabadiriko 575 ambao ni wanaume na wavulana.
|
WAANDISHI wa habari wakiwa katika semina wilayani Kahama mkoani Shinyanga
iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Care International
Tanzania. |
Alifafanua miongoni mwa mawakala hao 250 ni vijana wa kiume kutoka Shule za Msingi na Sekondari katika Kata za Lunguya,Bugarama na Bulyanhulu zilizo Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama huku akibainisha lengo la mradi ni kutaka mabadiliko ya usawa wa kijinsia kati mwanaume na
mwanamke.
|
WAANDISHI wa habari wakiwa katika maelekezo ya vitendo. |
Mashobe amewaeleza waandishi wa habari kuwa mradi huo tangu
kuanza kwake umeweza kuleta mabadiliko kwenye baadhi ya familia na kupunguza
ndoa za utotoni ambapo ndani ya wilaya
ya Kahama zililengwa kata tatu za Lunguya,Bugar ama na Bulyanhulu na
lengo ni kuwafikia wasichana 8000.
|
WAANDISHI wa habari wakiwa katika mjadala wa vitendo. |
Aidha alisema Wanaume wamepewa kipaumbele kwenye mafunzo hayo
kutokana na kuhusika kwa asilimia
kubwa kwakufanya vitendo vya mfumo dume hivyo wameona watoe elimu ili
waweze kubadilika sambamba na mafunzo hayo
kutolewa kwa waandishi wa habari ili waweze kufikisha ujumbe.
Pia kwa upande wa
vijana wamekuwa wakitoa elimu
mashuleni kupitia vilabu vyao
vilivyoundwa ikiwemo vikundi vya burudani kufikisha ujumbe kwa wenzao.
|
MWANDISHI wa habari wa magazeti ya Habarileo na Dailynews mkoani Shinyanga Raymond Mihayo akichangia Mada. |
Hata hivyo Mwandishi wa habari wa magazeti ya habarileo Raymond Mihayo amesema kuwa mashirika mengi yamekuwa yakijikita katika halmshauri ya wilaya ya Msalala zaidi ambapo
hata katika halmashauri ya Ushetu bado kunachangamoto nyingi za
unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike.
|