Hayo yalibainishwa na
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Mohamed Abdul wakati akitoa taarifa fupi kwa Mkuu
wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyoitoa kwenye hafla fupi ya kuwapongeza wadau
ambao hujitokeza kuwasaidia vijana hao.
Katika hafla hiyo Abdul
alisema Kikundi hicho maarufu kwa VIWAKAMAHAZA,tayari kimeotesha miche Elfu
10,ikiwa ni maandalizi ya upandaji miti katika eneo hilo la
Bulyanhulu,itakayopandwa katika vijiji vya kata hiyo.
Aidha Mwenyekiti huyo
alisema vijiji vitakavyonufaika na mradi huo ni Busindi,Busulwaangili,Namba Tisa,Bushing’we,Lwabakanga pamoja na
Kakola,ambapo ndio makao makuu ya kikundi hicho.
Hata hivo Mwenyekiti huyo
alisema Kikundi hicho kina changamoto nyingi za kiuchumi kutokana na shughuli
yake kuu ya kufanya kazi za usafi katika
mji wa Kakola,huku kikiwa hakuna vitendea kazi na vyanzo vya mapato vyenye
uhakika.
Kufuatia hali hiyo Mkuu
huyo wa wilaya aliwataka vijana hao kuwa waaminifu katika kazi yao,kwani ndio
njia pekee ya kupata wahisani watakaoweza kuwasaidia ili waweze kujitania zaidi.
Mpesya kwa kuanzia aliwapa
mashine moja ya kisasa ya kufyatua tofari za gharama nafuu ambayo alisema
atawasaidia kuanzisha mradi wa ujenzi wa majengo mbalimbali ya Umma na watu
binafsi.
Pamoja na msaada huo
Mpesya aliwaonya vikali kuachana na siasa kwanza na kwa umri wao haujafikia
kufanya hivyo kwakuwa hivi sasa wanapaswa kuimarisha uchumi kwanza kuliko
kufanya siasa wakati hawana vipato na wengine kusotea hata mlo wa siku moja.