Friday, September 19, 2014

HALMASHAURI YABUNI MBINU YA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MKUU wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akitoa tofari la Saruji katika uzinduzi wa Mradi wa Halmashauri ya mji wa Kahama  kufyatua tofari 40,000 kwa lengo la kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete, kukamilisha ujenzi wa Maabara za Sekondari ifikapo Desemba mwaka huu. 

  HALMASHAURI ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga imetoa usaidizi kwa wananchi kuchangia shughuli za maendeleo baada ya
kubuni mbinu za kutekeleza agizo la rais la ujenzi wa maabara kila shule ya sekondari ya kata,kwa kufyatua na kusambaza matofari elfu 40 ya saruji.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Felix Kimario,katika uzinduzi wa mkakati huo utakaonufaisha shule za secondary 10 ambazo hazina maabara kati ya 16 zilizopo katika halmashauri hiyo,uliofanyika viwanja vya halmashauri hiyo.  

Kimario alisema ujenzi huo ambao ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililotolewa la kutaka kila sekondari nchi nzima  kuwa na maabara,katika halimashauri yake ya mji wa Kahama utakamilika ifikapo Desemba mwaka huu ambapo mbinu waliyobuni ya kufyatua tofari 40,000 itawasaidia wananchi kuinua maboma ya ujenzi huo.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Machibya Kiduramabambasi akibeba tofari la Saruji katika uzinduzi wa Mradi wa Halmashauri yake ya kufyatua tofari 40,000/-kwa lengo la kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete, kukamilisha ujenzi wa Maabara za Sekondari ifikapo Desemba mwaka huu. 



Alisema katika mpango huo kila kata itapatiwa matofari elfu nne ambayo kwa mujibu wa mhandisi wa halmashauri hiyo Msoka Msumba  yanauwezo wa kukamilisha maabara yenye vyumba vitatu pamoja na meza zake za ndani

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Machibya  Kiduramabambasi alisema mpango huo umeizinishwa na  baraza lake la Madiwani ikiwa ni njia mojawapo ya kuwapa nafuu wananchi ya kuchangia ujenzi huo ambao sasa nguvu zao sitatumika kwenye kujenga msingi pekee wa maabara hiyo

Kiduramabambasi alisema baada ya kukamilika kwa maboma hayo halmashauri hiyo pia itatoa shilingi milioni 10 kila kata yenye mradi zitakazo saidia  upauaji wa majengo hayo ambapo tayari kiasi cha sh. Milioni 100 kimetegwa.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Bensoni Mpesya aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia vizuri mradi huo wa ujenzi wa maabara ili majengo hayo yawe na ubora unaotakiwa

Mpesya alisema serikali haiwezi kukubali kuona fedha nyingi za wananchi zinatumika kwa ujenzi wa chini ya kiwango hivyo ni wajibu wa viongozi wote wakiwemo madiwani kuhakikisha wanasimamia mradi huo ili uwe wa mfano katika maeneo mengine

Kwa mujibu wa afisa elimu sekondari wa mji wa Kahama Annastazia Manumbu  halmashauri hiyo ina jumla ya shule za sekondari za kata 16 huku 10 hazina maabara kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wanafunzi elfu 6972 waliopo kwenye kata hizo.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI