Monday, September 22, 2014

SIMBA YAVUTWA SHARUBU DAR.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MSHAMBULIAJI Emmanuel Okwi akiwania mpira na mabeki wa Coastal Union
GONJWA la udhaifu wa safu ya ulinzi ya Simba SC,kutokuwa makini yameigharimu timu hiyo kuanza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kutoka sare ya kufungana bao 2 – 2 na timu ya Coastal Union ya Tanga katika pambano maridadi lililochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 


 Mfungaji bora msimu uliopita Hamis Tambwe akipachika bao lake la kwanza kwa msimu huu.


Kwa matokeo hayo yamezifanya timu kongwe za Tanzania ambazo ni watani wa jadi kutoanza michuano hiyo kwa kusuasua hasa baada wapinzani wa jadi wa Simba SC, Yanga SC kuanza kwa kipigo cha bao 2-0 kutoka Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao mawili, yaliyotiwa kimiani na kiungo Shaaban Kisiga ‘Malone’ na mshambuliaji, Amisi Tambwe, lakini baada ya dakika 90 matokeo yalikuwa 2 – 2.

 KIPA wa Coastal Union;Shaaban Kado akiondoa hatari langoni mwake

Mshambuliaji Emmanuel Okwi alionyesha thamani yake kwa kupika bao zote za Simba SC ,huku Shaaban
Kisiga akifunga bao zuri la kwanza kwa mpira wa adhabu dakika ya sita, baada ya Okwi kuangushwa nje kidogo ya boksi.

 EMMANUEL Anorld Okwi akichanja mbuga.



Mfungaji bora wa msimu uliopita, Mrundi Hamis Tambwe akaifungia timu yake bao la pili baada ya kuunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya Mganda, Okwi dakika ya 36.

Coastal Union nao walipoteza nafasi mbili nzuri za kufunga kipindi cha kwanza, kwanza dakika ya tatu baada ya Mkenya, Itubu Imbem kuunganishia juu ya lango krosi ya Hamad Juma na baadaye Joseph Mahundi akashindwa kuunganisha krosi mnamo dakika ya 29.Hadi timu zinaenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao 2 -0.

 KIKOSI cha Simba Sport Club kabla ya mpambano wake na Coastal Union


Kipindi cha pili, vijana wa Coastal Union “Wagosi wa Kaya” walibadirika na kuuteka mchezo. Mshambuliaji wa Uganda, Lutimba Yayo Kato aliifungia bao la kwanza Coastal dakika ya 69, akitumia udhaifu wa mabeki wa Simba SC kujisahau baada ya kiungo wao, Pierre Kwizera kuchezewa faulo.


Mabeki wa Simba SC walitulia kumsikilizia refa Jacob Adongo wa Mara apige filimbi baada ya Kwizera kuchezewa rafu, lakini ‘akakausha’ na Yayo akafunga. Coastal walizidisha mashambulizi hukku Simba SC nayo iliendelea kupeleka mashambulizi langoni mwa Wagosi wa Kaya.

 KIKOSI cha Coastal Union kilichoanza kupambana na Simba SC.



Uhuru Suleiman alikosa bao la wazi dakika ya 78 baada ya kutanguliziwa pasi nzuri na Okwi, lakini akiwa amebaki na kipa Kado, akapiga juu.


Mkenya Rama Salim aliisawazishia Coastal dakika ya 83 kwa mpira wa adhabu- baada ya beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuunawa mpira nje kidogo ya boksi.

 MFUNGAJI bora msimu uliopita Hamis Tambwe akijaribu kumtoka beki wa Coastal Union


Mshambuliaji Paul Kiongera aliyetokea benchi kipindi cha pili alirudi nje anachechemea dakika ya 88 baada ya kuumia kufuatia kugongana na kipa Kado hivyo kumpisha Amri Kiemba.

RAMADHANI Singano "Messi"akifanya jitihada za kumpiga chenga beki ya Coastal Union;Abdallah Mfuko.


Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Miraj Adam, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Pierre Kwizera, Haroun Chanongo/Uhuru Suleiman dk58, Shaaban Kisiga ‘Malone’, Amisi Tambwe/Paul Kiongera dk67/Amri Kiemba dk88, Emmanuel Okwi na Ramadhani Singano ‘Messi’.


Coastal Union iliwakilishwa na; Shaaban Kado, Hamad Juma, Sabri Rashid, Abdallah Mfuko, Hamisi Kibacha, Juma Lui, Suleiman Rajab/Yayo Lutimba dk49, Razack Khalfan/Ayoub Athumani dk49, Itubu Imbem, Rama Salim na Joseph Mahundi/Abbas Athumani dk69.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI