MKUU wa wilaya ya Kahama;Benson Mpesya |
MKUU wa wilaya ya Kahama
Benson Mpesya ametaka watuhumiwa wote wa makosa ya kuwapa mimba wanafunzi wa
shule za msingi na sekondari waliokuwa wamekamatwa na kisha kuachiwa huru na
mahakama kwa mazingira ya kutatanisha wakamatwe na kufunguliwa mashtaka upya.
Kauli hiyo aliitoa jana
mjini Kahama baada ya kuwepo malalamiko ya viongozi wa Kata za Bugarama,Lunguya
na Bulyanhulu wakidai mbele ya waandishi wa Habari waliotembelea eneo hilo
kwamba watuhumiwa wa kuwapa mimba wanafunzi hao wote wako huru.
OFISI ya Serikali ya Kijiji cha Igwamanoni |
Mmoja wa Viongozi hao
Mratibu Elimu Kata ya Bugarama Stanley Mbuta alisema hali ya watuhumiwa hao
kuachiwa huru na mahakama wakati ushahidi wa kutosheleza umetolewa inawatia
katika wakati mgumu juu ya usalama wa maisha yao.
Alisema watuhumiwa hao
baada ya kuachiwa huru hurudi kijijini na kuwaoa wanafunzi hao waliowapa mimba
baada ya kumaliza kesi zao hali ambayo inawakatisha tamaa ya kuendelea
kufuatilia watuhumiwa hao.
Nae Afisa Mradi wa shirika
la Care International kupitia mradi wa Wanaume na Wavulana kuleta usawa wa
kijinsia Gega Bujeje alisema katika Kata hizo wameweka mawakala wa kuleta
mabadiriko kwa kutoa elimu juu ya madhara ya ndoa za utotoni na kukatisha
masomo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI