Sunday, September 21, 2014

MAKUNDI YA WASICHANA CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akipiga makofi baada ya kumshuhudia mmoja wa wasichana waliokatisha masomo baada ya kupata Ujauzito akiendesha kifaa cha ujasiriamali alichompatia.


MKUU wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Evarist Ndikilo amewaasa wasichana kuepukana na vikundi visivyo na tija sambamba na kufanya vitendo vilivyo kinyume na maadili ambavyo vimekuwa kichocheo vya kujikuta wakipata mimba za utotoni. 


Akizungumza jana kabla ya kugawa vifaa vya ujasiriamali vilivyotolewa na Kampuni ya Pepsi{SBL} kwa wasichana waliojifungua katika umri mdogo, Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wasichana kujiepusha katika makundi yasiyofaa ambayo yamekuwa kichocheo cha kukatisha ndoto zao za maisha.

Alisema mbali ya kujiepusha kujitumbukiza na kujiingiza katika makundi hayo yasiyofaa pia ni wajibu kwao kutofanya vitendo vingine visivyofaa katika umri mdogo na jamii kwani baadhi vimekuwa vikiwafanya akina mama  wadogo bila kutarajia.

MENEJA wa Kampuni ya Pepsi Cola {SBL}Nicolaus Coetz waliofadhili vifaa vya Ujasiriamali kwa wasichna waliokatisha masomo kwa kupata mimba,akitoa neno.



Aidha aliipongeza Kampuni ya Pepsi Cola {SBL}kwa kuona tatizo la wasichana waliopata mimba katika umri na kukatisha safari yao ya masomo ambayo ndio ulikuwa msingi mkuu wa maisha yao,kuwawezesha vifaa vya ujasiriamali vitakavyowasaidia kumudu majukumu ya kulea na kujikwamua kiuchumi na familia zao.

Injinia Ndikilo alilipongeza Shirika lisilo la kiserikali  la Education For Better Living (EBLI) nchini,kwa kuanzisha mpango unaolenga kuwajengea uwezo watoto wa kike walioacha shule ili kuwapatia mafunzo mbalimbali yakiwemo ya Kompyuta , Ujasiriamali na Biashara.



MKUU wa Mkoa wa Mwanza,Injinia Evarist Ndikilo akitoa hotuba kwa wasichana waliopata mimba za utotoni.


“Shirika hili kupitia mradi huu limeonyesha kufanikiwa, na imekuwa  Second Chance kwenu mabinti kujikomboa kimaisha baada ya kuwa mmepoteza nafasi ya kupata elimu ya kawaida kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni,misaada hii itumieni vyema iwe mkombozi wa maisha yenu,”Alisema Injinia Ndikilo.
MKUU wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akibeba mtoto wa mmoja wa waichana 45 waliopatiwa vifaa vya Ujasiriamali.  




Alisema katika kutekeleza mpango wa “Kijana chagua Maisha” unaotekelezwa katika shule 10 za Jiji la Mwanza utasaidia kuwaelimisha vijana wa kike ili waweze kuepukana na mimba za utotoni na kusaidia kuendelea vyema na masomo shuleni.

Aliupongeza Mpango huo unaofanywa kwa ushirikiano baina ya EBLI na Kampuni ya SBC huku shabaha yake ikiwa ni kuwawezesha wamama wadogo (Young Mothers) waweze kujitegemea  na kufanya biashara ili kupata kipato na kujikwamua kiuchumi sambamba na utunzaji mazingira ya Jiji la Mwanza linaloshikiria rekodi bora ya ushindi wa usafi na mazingira kwa mara ya tisa..

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya SBC, Niclous Coetz, inashirikiana na jamii na kwa kuzingatia hilo imekuwa ikirudisha kwa jamii faida inayopata kupitia bidhaa zake za Pepsi ambapo mbali na kutoa vifaa hivyo itachangia gharama za utoaji elimu na uainishaji wa fursa za biashara na nyanja mbalimbali kwa kushirikiana na EBLI nchini.

Wito wangu kwa wananchi kuendelea kutupatia ushirikiano na kutuunga mkono kwa kununua na kutumia vinywaji vya Pepsi ili Kampuni ya SBC nayo iweze kurejesha faida yake kwa jamii kwa kuchangia miradi na shughuli mbalimbali ya maendeleo na kutoa msaada wa vifaa na kughramia wataalamu wa kutoa elimu ili kuwasaidia wananchi kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

Wasichana  45 Jijini Mwanza walioacha shule na kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali  ikiwemo kujifungua wakiwa na umri mdogo na kuwa mama wadogo wamewezeshwa  vifaa vya ujasiriamali na Kampuni ya Pepsi (SBC)  ili kumudu majukumu ya kulea na kujikwamua kiuchumi na familia zao.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI