Sunday, September 28, 2014

SERIKALI YAOMBWA KUZIKUMBUKA SHULE BINAFSI KUZIPATIA MISAADA YA KIELIMU.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MKUU wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akiongea na Wahitimu,wanafunzi,walimu na wazazi katika mahafari ya kumi ya Shule ya Sekondari ya Mhongolo Progressive.


KATIKA kuboresha elimu nchini,Serikali imekumbushwa kutozisahau Shule za binafsi kuzipatiwa misaada ya vitabu kama inavyofanya katika shule inazozimiliki.


Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mhongolo Progressive ya wilayani Kahama,Jeremiah Gunda wakati wa mahafari ya kumi ya kidato cha nne mbele ya mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya.

Mwalimu Gunda aliikumbusha serikali kuwa shule za binafsi ni wadau wakubwa katika sekta ya elimu nchini hivyo pindi inapopatikana fursa ya misaada ya vitabu vya kiada na ziada nazo zipatiwe kwa faida ya vijana wa Tanzania ambao wanasoma katika shule hizo za kulipia.
VIJANA walioghani shairi wakiwawakilisha wahitimu wenzao wakitoka kwa madaha ukumbini
Aidha Mkuu huyo wa shule aliwaasa vijana wa kidato cha nne kuwadhihirishia wazazi wao kuwa kwa kipindi cha miaka minne walikuwa wasikivu na watulivu kwa kufanya mithani yao ya mwisho kwa utulivu,amani na kujiamini ili kupata matokeo mazuri.
 MKUU wa Shule ya Sekondari ya Mhongolo Progressive,Jeremiah Gunda akisoma risala.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Benson Mpesya aliwataka wanafunzi daima wajitambue kwa kuzingatia masomo ambayo ndiyo dira ya maisha yao na kuleta tija kwa Taifa,hivyo ni vyema wakazingatia nidhamu na kujituma katika masomo kwa mustakabari wao mzuri kwa maisha ya baadaye.
 MKUU wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akitoa nasaha.
 "Msifikiri mpo hapa kwa bahati mbaya,bali wazazi wenu wanatimiza wajibu wao,hivyo waoneeni huruma kwa kuhakikisha mnafanya vyema katika masomo,kwani wamejidhurumu vitu vingi kwa ajili yenu,"Alisema Mpesya.
Add caption

 MKUU wa wilaya akimpongeza mmoja wa wahitimu.
Kwa upande wake Mwalimu Mwandamizi Taaluma katika Shule ya Sekondari ya Mhongolo Progressive,John Mbale alisema shule hiyo imeanzisha utamaduni wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vyema kwenye masomo yao nyakati za mitihani ya shule na ile ya Kitaifa.

Mbale alisema zawadi hizo zitachochea ushindani wa masomo kwa wanafunzi,hali itakayosaidia kunyanyua kiwango cha taaluma shuleni hapo na taifa kwa ujumla.
WANAFUNZI wa kidato cha tatu wakiserebuka.

Alisema katika kutekeleza utaratibu huo,kwa mwaka huu shule imetenga kiasi cha Shilingi 1,950,000/= zilizokabidhiwa kwa wanafunzi Ishirini na Sita wa kidato cha tatu,waliopatiwa Shilingi Elfu Hamsini kila mmoja.

Alisema wengine walionufaika na utaratibu huo kwa mwaka huu ni wanafunzi Kumi na sita wa kidato cha pili waliopatiwa fedha taslimu Shilingi Elfu Tano kila mmoja.. .
 WAHITIMU wa kidato cha Nne wakiserebuka

Wahitimu katika sekondari hiyo wanaotarajia kuanza mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne,walikuwa wanafunzi sitini na tisa,huku wasichana wakiwa Ishirini na Sita na Arobaini na tatu ya watoto wa kiume.
 WAHITIMU wa kidato cha nne wakiimba kwa bashasha

WAHITIMU wa kidato cha Nne.


KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI