MASHABIKI wa Ndanda FC wakishangilia wakati wa mapumziko kwa kuonyesha ishara ya vidole vitatu |
WAGENI wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ndanda FC wameanzia kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Stand United katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Katika
mchezo huo wa ufunguzi uliochezeshwa kwa umahiri
mkubwa na Mwamuzi Hashim
Abdallah kutoka Dar Es Salaam,hadi mapumziko Ndanda walikuwa wakiongoza kwa bao
3 – 1.
Katika
pambano hilo lililokuwa zuri la kuvutia,huku wageni wakionyesha soka la kuvutia
zaidi,walifanikiwa kujipatia bao la kuongoza mnamo dakika 16 ya mchezo
lililofungwa kwa umaridadi mkubwa na Paul Ngalema.
TIMU ya Ndanda FC wakiwa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga |
Bao la pili timu hiyo inayodhaminiwa na Bin Slum kama ilivyo Stendi United dakika 35 ya mchezo na Nassoro Kapama na dakika moja baadaye Stendi United ilijipatia bao la kufutia machozi kupitia kwa Salum Kamana,na lile la tatu kwa Ndanda FC lilifungwa na Ernest Joseph Mwalupani mnamo dakika ya 40.
Na bao
la Nne la vijana hao liliwekwa kimiani na Elius Ndokezi dakika ya 90 ya mchezo.
NI Stendi United kabla ya pambano kati yake na Ndanda FC kuanza |
WAKATI HUOHUO;Azam FC wameanza utetezi wa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kishindo baada ya kuwafunga Polisi Moro kwa jumla ya Bao 3 – 1.
Ikicheza
katika uwanja wake wa Nyumbani wa Azam Complex uliopo Chamazi,Azam
FC walitawala mchezo huo kwa kiwango kikubwa na walijipatia mabao yake kupitia
kwa Mrundi Didier Kavumbagu aliyecheka na nyavu mara mbili huku moja
likipachikwa wavuni na Nahodha wa timu hiyo Agrey Moriss.
Wakati
Polisi Moro ambao wamerejea Ligi Kuu msimu huu walijipatia bao lao kupitia
kwa Nahodha wao Bakari Sorry.Na katika
uwanja wa Sokoine,Maafande wa JKT Ruvu wamedhihirisha kuonyesha ushindani
katika Ligi ya Msimu huu baada ya kutoshana nguvu na washindi wa tatu wa Ligi
Kuu msimu uliopita timu ya Mbeya City.
UTAMU wa Ushindi!Ni mashabiki wa Ndanda FC wakiserebuka baada ya timu yao kuondoka na ushindi wa bao 4 - 1 |
Timu
hizo zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza na kusababisha pambano hilo
kuwa la kuvutia na kusisimua kutokana na timu zote kucheza soka zuri,
Kipindi
cha pili Mbeya City walicharuka kwa wachezaji wake kuonyesha kupania kuondoka
na ushindi lakini hadi mwisho wa mchezo hakuna aliyetikisa nyavu za mwenzake.
Nao
Prisons FC wamewapigisha kwata maafande wenzao wa Ruvu Shooting kwa
kuwatungua bao 2 – 0 katika pambano lililochezwa uwanja wa Mabatini
Mlandizi,Pwani.
|
MATOKEO YA MICHEZO YA
UFUNGUZI WA LIGI
Azam FC 3-1 Polisi Moro
Stand Utd 1-4 Ndanda FC
Mgambo 1-0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 0-2
Prisons
Mtibwa Sugar 2-0 Yanga
Mbeya City 0-0 JKT Ruvu