Sunday, September 21, 2014

JAJA MWISHO MSAMVU,MOROGORO NI MGOSI NA AME ALI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO





Kipigo cha kwanza; Kocha Marcio Maximo ameanza vibaya Ligi Kuu Bara


                             
KOCHA Marcio Maximo akitoa maelekezo kwa Jaja.
KOCHA Mbrazili;Marcio Maximo akiongoza Yanga SC kwa mara katika mechi ya Ligi Kuu  ya Vodacom Tanzania Bara ameanza vibaya kwa kupokea kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Kwa matokeo hayo yamepoteza ndoto ya Kocha huyo ya kutwaa Ubingwa pasipo kupoteza mchezo,huku mshambuliaji wa timu hiyo Genilson Santana ‘Jaja’ambaye kabla ya kuanza michuano hiyo jina lake lilitawala midomoni mwa mashabiki wa soka nchini kwa umahiri wake wa kuzifumania nyavu;akikosa penalti.

Katika pambano hilo lililokuwa kali na la kuvutia hadi mapumziko,Mtibwa Sugar walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na DC Motema Pembe ya DRC, Mussa Hassan Mgosi dakika ya 16 aliyemalizia pasi ya kichwa ya Ame Ali na kumuwahi kipa Deo Munishi ‘Dida’ aliyetokea vizuri kutaka kudaka. 

Baada ya bao hilo, nyuki wakaingia uwanjani jambo lililosababisha wachezaji walale chini kwa dakika mbili, kabla ya wadudu hao kuondoka na mchezo huo uliochezeshwa na refa Dominick Nyamisana wa Dodoma, aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Milambo Tshikungu wa Mbeya, kuendelea.


Dakika ya 32 ya mchezo mshambuliaji tishio wa Yanga Genilson Santana ‘Jaja’ almanusura aipatie bao la kusawazisha timu yake baada ya kuunganisha vizuri kwa kichwa kona ya Haruna Niyonzima, lakini mlinzi Hassan Ramadhani alikumbushia vitu adimu vilivyokuwa vikifanywa na kisiki cha zamani cha timu ya Taifa na Simba Sport;George Masatu kwa kuokoa mpira uliokuwa  unaelekea nyavuni.


Kipindi cha Pili kilipoanza tu,Yanga ilifanya shambulio kali na kufanikiwa kupata penalti baada Salim Mbonde kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, lakini kipa Said Mohamed Kasarama akapangua kwa mguu mkwaju wa Jaja.


Yanga ilitikisa nyavu za Mtibwa Sugar katika dakika ya 47 ya mchezo,kwa bao lilifungwa Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Hamisi Kiiza ‘Diego,lakini refa akasema aliotea. Na mnamo dakika ya 49 tena, Mrisho Ngassa alifunga bao lakini refa alilikataa kwa madai kuwa pia aliotea.


Mnamo dakika ya 67,pambano hilo lilisimama kwa sekunde kadhaa baada ya Simon Msuva kuvamia lango la Mtibwa na kutoa vitu vilivyokuwa chini upande wa nyavu kubwa na kukimbia navyo huku akikimbizwa na kipa Said Mohamed Kasarama kabla ya kuvitupa nje.


Dakika ya 82 mpishi wa bao la kwanza, Ame Ali aliifungia Mtibwa bao la pili baada ya kufanikiwa kuwahadaa mabeki wawili wa kati wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannaaro’ na Kevin Yondan kisha kumtungua Dida kufuatia pasi nzuri ya Hassan Ramadhani.


Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende/Majaliwa Shaaban dk64, Salim Mbonde, Andrew Vincent, Shaaban Nditi, Ali Shomary, Muzamil Yassin, Ame Ali, Mussa Mgosi/Vincent Barnabas dk50 na Mussa Nampaka/Dickson Daud dk72.
 
Kwa upande wa Yanga SC,kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Omega Seme, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Said Bahanuzi dk72, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/Simon Msuva dk46. 

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI