Hadi sasa ugonjwa huo umeishauwa nusu ya wagonjwa 6,000 waliokwishaambukizwa,huku Umoja wa Mataifa ukisema idadi ya maambukizi mapya imevuka na kuwa
maelfu badala ya mamia kwa wiki.
Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na Virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu "Ebola Virus" Ugonjwa wa damu kutoganda, ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinaazosababisha kutokwa na Damu mwilini,(Viral Haemorrhagic Fevers) Chanzo kamili cha virusi vya ugonjwa
huu hakijulikani. Katika orodha ya watu 10 waliopata kirusi cha Ebola, basi wastani kati ya watano au tisa hufa.
Maradhi hayo yamezikumba nchi hizo za Afrika Magharibi,huku madaktari mbalimbali duniani wakijitahidi kuwanusuru wagonjwa sambamba na jitihada zikifanyika za kudhibiti kutoenea kwa maradhi hayo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI