Mvutano
huo ulisababisha Polisi kuingilia kati na kuwatawanya wafuasi hao kisha
kuwaruhusu CUF wafanye mkutano wao kwa kuwa ndiyo waliokuwa na kibali
halali.
Kamanda
wa Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema vurugu hizo zilidhibitiwa na
Polisi waliowaondoa wafuasi wa CCM ambao hawakuwa na kibali halali.
Mashuhuda
walisema ilikuwa vurugu kwa wafuasi wa CCM na CUF baada ya kupigana kwa
kutumia viti na mawe na kwamba polisi walizuia vurugu hizo kwa mabomu
ya machozi.
Mmoja wa viongozi wa CUF, Mohamed Mluya alisema walipewa kibali cha kufanya mkutano huo jana.
Alisema waliwaonyesha kibali chao lakini wafuasi wa CCM walionyesha kibali kilichoonyesha kuwa walipaswa kufanya mkutano Ijumaa.
Mluya alisema wafuasi hao walitaka kufanya mkutano jana bila kubadilisha kibali.
via>>Gumzo la jiji
via>>Gumzo la jiji