kwa lengo la kupinga kuendelea kwa bunge maalum la katiba linaloendelea mjini DODOMA.
Akizungumza na wafuasi wa chama,Mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani wilayani Kahama Robert Sewondo alisema maandamano hayo hayapo kisheria hivyo akawataka kutawanyika kabla ya jeshi la polisi halijatumia nguvu kuwatawanya.
Alisema jeshi la polisi limepiga marufuku mikutano na maandamano kwa chama hicho kutokana na kuwepo kwa dalili za uvunjifu wa amani hivyo wanapaswa kutii sheria bila shurti.
Katika maandamano hayo
ambayo kulikuwa na wafuasi wengi wa chama hicho waliokusanyika katika ofisi za
wilaya za chama hicho kuanzia saa moja asubuhi yakiongozwa na Mwenyekiti wa
Chama hicho Juma Protas na baadhi ya madiwani wa chama hicho wakiwa wamejifunga
vitambaa vyeupe mikononi mwao kuashiria amani.
Wafuasi hao waliokuwa na mabango mbalimbali yanayolaani seriakali mabango hayo miiongoni yakisomeka; “Serikali ya CCM inachofanya ni utapeli mtupu.Bunge la Katiba ni mpango wa wizi mtupu ole wenu 2015.”pia “Kikwete ,Samweli 6 Ufedhuli wa kufuja fedha za Watanzania kwa kigezo cha Bunge la Katiba acheni mara moja”na mengine kibao,walianza maandamano hayo rasmi mnamo saa tatu asubuhi.
Wakiwa katika maandamano ambayo yalitawaliwa na utulivu wakianzia katika ofisi zao za chama wakiwa na vitambaa vyeupe walivyovaa kichwani na mikononi ghafla ziliibuka gari nne za polisi zilizokuwa na askari zikiongozwa na PT 0841,walifika na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi hao,hatua ilileta mparanganyiko mkubwa.
Aidha baada ya Polisi hao
waliokuwa na silaha zilizowaogofya wafuasi hao wa CHADEMA na kumudu kuwatawanya, walifanikiwa kuwatia mbaroni viongozi
watatu wa Chama hicho ambao ni Mwenyekiti wa wilaya,Juma Protas,Diwani wa Kata
ya Nyihogo,Amosi Sipemba na Diwani viti maalumu Winfrida Mwinula.
Hata hivyo kabla ya
kukamatwa Mwenyekiti wa Chama hicho alisema Bunge la Katiba kusimamishwa mara
moja kinachofanyika Dodoma hakiwezi kupelekea kupata Katiba ya Watanzania.
Alilaani kitendo cha polisi kutumia silaha za vitisho kuwatawanya watu ambao hawakuwa
na silaha wala kuashiria uvunjifu wa amani,huku akisisitiza kuwa serikali
imepiga marufuku maandamano kwa ujumla wake lakini uongozi wa chama chake
wilaya uliandika barua ya kutoa taarifa kwa mujibu kanuni na sheria ya vyama
vya siasa.
“Katiba inaturuhusu kutoa
taarifa kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza,hatua ambayo tuliietekeleza lakini
Jeshi la Polisi halikutoa majibu kama limeyazuia maandamano hayo”,Alisema
Protas.
Alisema anashangazwa na
Jeshi hilo kuleta askari wengi wakiwa na silaha za moto na mabomu ya mchozi na magari manne
jambo ambalo lingeweza kujibiwa kwa maombi ya barua kama waliyoiwakilisha kwa jeshi hilo.
Nae Diwani wa Viti Maalumu
Winifrida Mwinula alisema kuwa Bunge hilo linaendelea kula fedha za wananchi
jambo ambalo mbunge mmoja katika Bunge la Katiba analipwa shilingi Laki saba
kwa siku jambo ambalo mwananchi wa kawaida anashindia mlo mmoja duni kwa siku
huku wao wakiendelea kuneemeka huku wananchi wa kawaida wakiwa na maisha duni.
Kwa upande wake Diwani wa
kata ya Nyihogo Amosi Sipemba
alisema kuwa jambo la maandamano lilpo kikatiba na
Chadema wanachokiona katika Bunge la Katiba halina manufaa kwa wananchi hasa
kwakuwa linapindishwa pindishwa na kuona kinachofanyika ni ufisadi mtupu.
Pia mfuasi mmoja wa chama
hicho Injinia Tadeo Joachimu alisema kuwa inashangaza jeshi la polisi
kuyaingilia wakati yapo Kikatiba,na kukilaani chama cha mapinduzi kutumia dola
kukiangamiza CHADEMA jambo ambalo alidai ukiukwaji wa Katiba.