Maandamano
hayo yaliokuwa yaliyokuwa yametangazwa na CHADEMA Mkoa wa Shinyanga yalipangwa kufanyika
jana kuanzia saa mbili asubuhi,licha ya kupigwa marufuku na Polisi,hayakuonyesha
dalili ya kuwepo baada katika ofisi za chama hicho kutofunguliwa na kukosekana
kwa kiongozi yeyote.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga;Peter Machanga akiongea kwa simu
alidai tangazo lao la kufanyika maandamano hayo lilikuwa la kuwaandaa wananchi
kwa ajili ya maandamano yatakayotangazwa rasmi siku zijazo.
Kwa
upande wao wakazi wa Shinyanga Mjini walisema maandamano hayo huenda
yameshindikana kufanyika kutokana na askari wa jeshi la Polisi kutapakaa
mitaani tangu asubuhi sana ili kukabiliana na mfuasi yeyote wa chama hicho ama
mwananchi yeyote atakayejitokeza kuandamana.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI