ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi wa Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Emmanuel Makala akiweka jiwe la Msingi la Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Agape wilayani Kahama. |
kujenga Shule ya Sekondari ya Ufundi itakayotoa mafunzo ya stadi za maisha.
Hayo yalielezwa na Mkuu wa Jimbo la Kusini
Magharibi;Mchungaji Daniel Mono katika taarifa aliyoisoma mbele ya Askofu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Askofu
Emmanuel Makala,wakati wa
kuweka Wakfu ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Agape Lutheran.
kuweka Wakfu ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Agape Lutheran.
Mchungaji Mono alisema ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Agape utakayojengwa kwa awamu nne utagharimu jumla ya Shilingi 520,623,740/= ambapo shule hiyo itakuwa msaada mkubwa wa kumudu kujitegemea kimaisha kwa vijana watakaobahatika kusomea shule hiyo.
Alisema lengo kubwa la
kuanzishwa kwa sekondari hiyo ni kuwapatia wanafunzi masomo ya ziada ya ufundi
ambayo ana hakika yatakuwa mkombozi mkubwa wa kuondokana na maisha ya utegemezi
kama walionayo vijana wengi waliokomea kidato cha nne.
MCHUNGAJI Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi,Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria;Daniel Mono akisoma taarifa ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Agape. |
Mchungaji huyo alisema
matarajio ya Sekondari hiyo ni kuanza January 2016,ambapo mbali na kuwajengea
vijana stadi za maisha ili kuondokana na dhana ya kuajiriwa pia itakuwa msaada
mkubwa kwa maendeleo ya Dayosisi kwa kuongeza samani na majengo pindi
wanapokuwa katika mafunzo ya vitendo.
WAAMINI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania "KKKT"wakiwa katika Wakfu ya Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Agape katika Kata ya Mwendakulima wilayani Kahama. |
Awamu ya tatu itakuwa ni
kujenga jengo la Utawala na Karakana ya ufundi itakayogharimu pia Shilingi
150,000,000/= huku awamu ya mwisho itakayohusu nyumba za walimu ambazo
zitagharimu Shilingi 120,000,000/= hivyo kuwaomba wafadhili na marafiki wa
kanisa kujitokeza kuchangia ili kukamilisha kwa wakati sekondari hiyo.
WAAMINI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
"KKKT"sambamba na wageni wao wa Shirika la Most Ministries Team kutoka nchini Marekani wakiwa katika Wakfu ya Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Agape
katika Kata ya Mwendakulima wilayani Kahama.
Nae Askofu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania “KKKT”Jimbo la Kusini Magharibi;Emmanuel Makala
aliwaasa watakaosimamia ujenzi huo kuwa waadirifu na kuhakikisha mradi huo
unakuwa na akaunti yake isiyoingiliana na ya miradi mingine ya Kanisa.
Askofu Makala katika kuhakikisha
hilo linafanyika alianzisha Harambee ya ufunguzi wa akaunti hiyo ambapo
zilipatikana kiasi cha Shilingi Milioni Moja taslimu.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI