MKUU wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya. |
CHANGAMOTO kubwa inayokutana nayo serikali ya wilaya ya Kahama katika
kudhibiti mauaji
ya vikongwe kwa kuwatia mbaroni wauaji kusudi sheria ichukue
mkondo dhidi yao ni kukosekana kwa viongozi wa vijiji waadirifu ambapo pindi matukio
hayo yanapojitokeza huyageuza kuwa vitega uchumi vya kuwaingizia pato..
Mkuu wa Wilaya ya Kahama;Benson Mpesya alisema kushamiri kwa matukio hayo ya mauaji kwa
kukatwa mapanga kwa akina mama katika mikoa ya Shinyanga na Geita.
Kwa asilimia kubwa kunasababishwa na viongozi wa serikali za
vijiji ambao hukosa uzalendo kutokana na kugeuza matukio hayo kuwa vyanzo
vya mapato yao kwa kuwahifadhi watuhumiwa wa vifo hivyo ambavyo hudaiwa
husababishwa na imani za kishirikina..
Mkuu huyo wa wilaya, aliwashutumu viongozi wa serikali za vijiji kwa kutokuwa waadirifu na
kusahau miiko yao ya uongozi kwa kuwakumbatia wauaji wa akina mama ambao wengi
huuawa kuanzia miaka 45 huku wakitambua fika tabia hizo zinakwamisha
jitihada za serikali za kuwatia mbaroni na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika
hao.
Alisema mauaji hayo huwa vitega uchumi wa viongozi wa serikali za
vijiji wa eneo lililotokea tukio ambapo hushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi
la Polisi badala yake huchukua fedha kwa wauaji ili wawahifadhi hivyo kufanya
vita dhidi ya mauaji ya kuwakata mapanga akina mama kwa imani za kishirikina,kuendelea kuwa janga
kubwa pamoja na viongozi mbalimbali wa dini na serikali kupigia kelele ya hali
hiyo.
.
Mpesya alisema upo ushahidi wa kutosha kwa baadhi ya matukio ya
mauaji ya vikongwe yanapo tokea ,mara nyingi wenyeviti wa vijiji hubaininka kuwaficha
watuhumiwa wa mauaji, na tayari mwenyekiti mmoja ameshikiliwa (hakumtaja
jina) baada ya kub ainika kupokea shilingi million tatu (3,000,000) kutoka kwa
watuhumiwa wa mauaji ili awahifadhi.
Aidha kuhusu kukwama kwa
kesi hizo mahakamani pindi watuhumiwa wanapofikishwa mbele ya sheria kunatokana
na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani watuhumiwa wa mauaji
hayo baada ya mashahidi kuepuka kutoa ushahidi kwa hofu nao kukumbwa na mauti
kutoka kwa baadhi ya wauaji hao ambao
wanakuwa hawajakamatwa.
Pia alisema wapo wasamalia wengine hujitolea kutoa ushahidi lakini
wengi wao wamekimbia familia zao au kuhama kabisa maeneo yao kwa vitisho
mbalimbali ambavyo hutolewa na baadhi ya wauaji, hali ambayo pia imechangia kwa
watu wanao wafahamu wauaji hao kushindwa kujitokeza hadharani kutoa ushahidi
Hata hivyo serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kutoa elimu juu
ya umuhimu wa ushahidi katika kesi za mauaji hayo ambayo pamoja na kuwa ya
hatari lakini wauaji wanajulikana ni kikosi cha kukodi kati ya shilingi laki
tatu hadi tano kwa kuua mtu mmoja .