MWITO umetolewa kwa wanaume
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, kutumia dawa za kupunguza makali ya Virusi
vya Ukimwi, ili kukabiliana na maambukizi mapya ya maradhi hayo.
Mwito huo litolewa na Shirika la
Afya Duniani “WHO”ambapo lilieleza umuhimu wa wa wanaume hao kutumia dawa hizo
za kupunguza Virusi vya Ukimwi “ARV’s”hata kama hawajabainika hawajabainika
kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi “ HIV”.
Shirika hilo linasema kuwa ikiwa
wanaume hao watatumia dawa hizo za kuzuia maambukizi pamoja na kutumia Condom,
huenda ikapunguza maambukizi ya HIV miongoni mwao kwa zaidi ya asilimia 20.
Msemaji wa shirika hilo, alisema
kuwa kiwango cha maambukizi miongoni mwa wanaume wapenzi wa jinsia moja, watu
wanaotumia madawa ya kulevya , wafungwa na makahaba imeongezeka.
Kikundi hicho cha wanaume ndicho
kilichoanza kuambukizwa HIV miaka 33 iliyopita.
Miaka ya zamani dunia ilipoanza
kuchukua hatua dhidi ya maradhi ya ukimwi kutokana na picha zilizokuwa
zinatisha za wagonjwa wa Ukimwi, ripoti ya shirika hilo inasema kizazi cha leo
hakijali sana kuhusu ugonjwa huo hasa kwa sababu kuna dawa za kupunguza makali.
Kwa mujibu wa WHO, haali hii
inatishia juhudi dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.
Kizazi cha leo kinakabiliwa na
hatari ya kuambukizwa HIV zaidi ya maradufu. Mfano nchini Bangkok, idadi ya
wanaoishi na virusi vya HIV kwa wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, ni
5.7%.
Katika mapendekezo yake mapya ,
shirika hilo linataka wanaume waanze kutumia dawa za kupunguza makali ya HIV
kama njia ya kujikinga kutokana na maambukizi
Chanzo cha Habari:- BBC