VIJANA chini ya miaka Kumi wakifukuza kuku,katika bonanza lililoandaliwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine Ltd,kupitia Mgodi wake wa Buzwagi. |
KAMPUNI ya uchimbaji
madini ya African Barrick Gold kupitia mgodi wake wa dhahabu wa Buzwagi umepongezwa kwa kuwa karibu na
wananchi wa Kahama katika shughuli mbalimbali za Maendeleo sambamba na
uhamasishaji katika sekta ya michezo hatua itakayosaidia kukuza uchumi.
Pongezi hizo zilitolewa na
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Benson Mpesya katika kilele cha Bonanza la michezo sambamba na
hitimisho la ufadhili uliotolewa
wa kutazama bure michuano ya Kombe la Dunia kwa wananchi wa mji wa Kahama na Mgodi
wa Dhahabu wa Buzwagi.MTOTO Catherine,mwanafnzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Majengo akipongezwa na Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi;Dorothy Bikurakule baada ya kuibuka na ushindi wa kukimbiza kuku. |
Alisema kampuni hiyo imeonyesha
nia ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama kwani mbali na kuandaa bonanza
hilo pia wanatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa
barabara za lami,shule,zahanati na vituo vya afya.
VIJANA wakichuana mbio za Mita 200 za kukimbia na gunia |
“Hatuna budi Mwekezaji
huyu kumfanya ni mwenzetu,kwa maendeleo anayotufanyia kama miundo mbinu ya
barabara maana yake wote tunafaidika na dhahabu,tushikamane naye na tumtumie kusonga
mbele kichumi ili wilaya yetu kwenda na wakati,”Alisema Mpesya.
GOLIKIPA wa timu ya Bodaboda FC;Charles Alphonce akipangua mchomo wa penalti |
“Hatuna budi Mwekezaji
huyu kumfanya ni mwenzetu,kwa maendeleo anayotufanyia kama miundo mbinu ya
barabara maana yake wote tunafaidika na dhahabu,tushikamane naye na tumtumie kusonga
mbele kichumi ili wilaya yetu iweze kwenda na wakati,”Alisema Mpesya.
MKUU wa wilaya ya Kahama;Benson Mpesya akiwaongoza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama;Felix Kimario mwenye shati la maua na mwenye T'Shirt ya kijani ni Amosi John mwakilishi wa Mgodi.
Alisema hatua iliyofanya
Mgodi kufunga Luninga kubwa katika uwanja wa michezo wa Halmashauri ya Mji,kwa
lengo kuwasaidia wananchi wasio na kipato
kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia bure.,pia iliwakusanya mashabiki wa
mchezo huo pasipo kujali uwezo wa kipato jambo lililozidisha upendo miongoni
mwa wana Kahama.
MKUU wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akisalimiana na waamuzi wa pambano la Fainali ya Bonanza. |
MASHABIKI wa Bodaboda FC wakishangilia ushindi. |
Kaimu
meneja mkuu mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi Amos John alisema African Barrick Gold
wataendelea kushirikiana na jamii ya Kahama ili kujenga undugu na kuimarisha
upendo,umoja na mshikamano katika kuhakikisha kuwa jamii ya Kahama na kampuni
hiyo wanafanikiwa pamoja.
NI furaha tu kwa mashabiki wa Bodaboda FC na mashabiki wao |
Alibainisha
kuwa Lengo la Brazuka Bonanza
ni African Barrick kuhamasisha umoja,ushirikiano na upendo katika kuhakikisha kuwa mgodi na jamii
zinafanikiwa kwa pamoja hasa katika kuhamisha michezo hususani soka ambao
kwa karne ya sasa ni ajira.
Katika mchezo wa fainali
wa Bonanza hilo lilidumu kwa siku tatu na kushirikisha timu nane.Timu ya Bodaboda FC iliibuka kinara wa
michuano hiyo ya Brazuka Soka Bonanza baada ya kuibanjua timu ya Afya FC kwa bao 5 – 3..
MKUU wa wilaya ya Kahama Bensoni Mpesya akimkabidhi Kapteni wa Mabingwa wa Bonanza hilo kutoka timu ya Bodaboda bahasha yenye Shilingi Laki Tano. |
Pambano hilo lililokuwa la kuvutia lilitimua vumbi katika dimba la
Halmashauri ya Mji wa Kahama na kuhudhuriwa
na mamia ya wapenda soka michezo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama;Benson
Mpesya,hadi dakika 90 zinaisha matokeo yalikuwa sare ya bao 2-2.
KATIKA Usiku wa Brazuukaaa,Christian Bella alitoa burudani kamambe. |
Mabao yakiwa yamepachikwa nyavuni na Baraka Juma na Benjamini Petro kwa
upande wa Bodaboda FC,na Ramadhani Ramadhani na Dokta Castro Obote kwa upande
wa timu ya Afya FC,ndipo ilipotumika sheria ya mikwaju ya penati,na mabingwa wa
bonanza hilo kutumbukiza kimiani bao 3.
KATIKA Usiku huo Msanii Nay wa Mitego alimuibua Diamond wa Kahama na kutoa naye shoo ya kibao;MUZIKI GANI? |
Penalti zilizofungwa kiustadi na Said Athumani,Baraka Juma na Deogratias
Christian,huku kwa upande wa Afya FC, Dokta Castro akifanikiwa kupachika
nyavuni goli moja huku wengine michomo yao ikiokolewa kwa ufundi na kipa wa
Bodaboda;Charles Alphonce.
NAY wa Mitego na Diamond wa bandia walikamua ipasavyo na kuzipa burudani ipasavyo nyoyo za waliohudhria Usiku huo wa Brazukaa. |
Kwa Ubingwa huo Bodaboda FC inayoundwa na Wajasiriamali waendeshao
pikipiki kibiashara walijinyakulia Kitita Cha Shilingi Laki Tano na mpira,na
washindi wa pili timu ya Afya FC wakipatiwa Shilingi Laki Mbili na Daladala fc wakipata
shilingi laki 1.
NAY wa Mitego akishambulia Jukwaa ipasavyo. |
Hata
hivyo timu zote nane zilizoshiriki mashindano hayo zilipewa mpira mmoja kila
timu,isipokuwa timu ya Wasanii fc ambayo ilinyimwa mpira kutokana na utovu wa
nidhamu baada ya kususia mechi ya kutafuta mshindi wa tatu iliyopangwa kuchezwa
asubuhi.
Katika
bonanza hilo pia kulikuwepo michezo mingine kama kufukuza kuku kwa vijana wa
rika lote wasichana kwa wavulana na kukimbia na magunia,na baada ya bonanza
hilo kulifatiwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki Christian Bella na Nay wa
Mitego kabla ya kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI