MJASIRIAMALI Chausiku Mashamba [15]mkazi wa kijiji cha Kishula,Kata ya Chona katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu akichangia hoja kwenye somo la Ujasiriamali kabla hawajapatiwa fedha zao. |
MKURUGENZI wa Shirika la HUHESO FONDATION lenye makao Makuu yake Kata ya Malunga,Juma Mwesigwa akizungumza na Vijana Wajasiriamali 15 kabla hawajapatiwa fedha zao za mitaji. |
NAE Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi Halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Morgan Mwita alipata wasaa wa kuzungumza na vijana wajasiriamali waliopatiwa fedha za mitaji |
MJUMBE wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Kulwa Shoto akiongea na vijana Wajasiriamali |
MKURUGENZI wa Shirika lisilo la Kiserikali la Rafiki,Gerald Ng'ong'a akifundisha somo la Ujasiriamali kwa vijana Wajasiriamali kutoka Kata 15 za Halmashauri ya wilaya ya Ushetu. |
MJUMBE wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Diwani Kulwa Shoto akimkabidhi fedha ya mtaji Shija Fedrick [18]mkazi wa Kata ya Uyogo. |
MWITO umetolewa kwa
vikundi vya vijana kuhakikisha pesa za ujasiriamali wanazopatiwa ziwe chachu za
kuwaendeleza kiuchumi na zisiwe sababu ya kuwa kichocheo kwao cha kupata maambukizi
mapya ya UKIMWI.
Hayo yalielezwa na Mjumbe
wa Kamati ya kupambana na maambukizi ya Ukimwi katika Halmashauri ya wilaya ya
Ushetu;Kulwa Shoto wakati wa kukabidhi Shilingi Milioni Moja na Nusu kwa vijana
Wajasiriamali 15 kutoka Kata 15 za Halmashauri hiyo.
Shoto ambaye ni Diwani wa
Kata ya Bukomela wilayani Kahama alimuwakilisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo;Tabu
Katoto,aliwaasa vijana wanaopata fursa ya mitaji ya Ujasiriamali kuhakikisha
wanazitumia fedha hizo kwa tija kwa kuanzisha na kuendeleza biashara ili
kuboresha uchumi wao.
Alionya vijana kutumia
mitaji ya ujasiriamali kwa vitendo vya anasa ambavyo havitawakomboa na lindi la
umaskini zaidi ya vitendo hivyo kuwa hatarishi kwao kiuchumi na kuwaingiza
katika janga la kupata Virusi vya Ukimwi.
Kwa upande wake Mratibu wa
kudhibiti Ukimwi katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu Morgani Mwita alisema
fedha hizo zinazotolewa kwa vijana kuwa mitaji pindi zikitumika kwa malengo
yaliyokusudiwa zitaliletea tija taifa na kusaidia kupambana na Maambukizi mapya
ya Ukimwi.
Nae Mkurgenzi wa Shirika
la HUHESO Foundation la wilaya ya Kahama,Juma Mwesigwa alisema japokuwa shirika
lake limetoa kiasi kidogo kwa Vijana Wajasiriamali lakini kikitumika kwa
malengo yaliyokusudiwa itakuwa msaada mkubwa kwa vijana hao kujiomboa Kiuchumi.
Aidha alisema Shirika lake
halitawatelekeza vijana hao bali litawafuatilia kwa umakini kuhakikisha fedha
hizo zinawapatia tija ikiwa ni sambamba na kubaini changamoto wanazokabiliana
nazo katika kutekeleza ujasiriamali na kutafuta njia ya kuwakwamua na
changamoto hizo.
Shirika la HUHESO
Foundation la wilayani Kahama chini ya ufadhili wa Halmashauri ya wilaya ya
Ushetu,limetoa Shilingi Milioni Moja na Nusu kwa vijana 15 kutoka katika Kata
15 za Halmashauri ya Ushetu ili kuwawezesha kufanya shughuli zitakazo wawezesha
kuboresha maisha yao.