BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO
|
WAKIWA na Nyuso za bashasha ni Miss Redd's Shinyanga 2014;Nicole Sarakikya[21] katikati,Mshindi wa Pili,Mary Bugingo[20] na Mshindi wa tatu Rachel Mushi mwenye gauni la kijani. |
|
Warembo 20 wakikamua jukwaani katika Shindano la kumpata Miss Redd's Shinyanga 2014. |
|
WAREMBO Jackline Robert kushoto na Nilam Siraji wakitembea kwa madaha jukwaani ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kinyang'anyiro cha kuwania taji la Miss Redd's Shinyanga 2014. |
|
WAREMBO waliobahatika kuingia Kumi bora katika mchuano wa kumpata Miss Redd's Shinyanga 2014. |
|
WAKIWA wameshikana mikono na nyuso za shauku ni Warembo Nicole Sarakikya kulia na Mary Bugingo wakisubiri kutangazwa kwa Mshindi wa Kwanza wa Kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Redd's Shinyanga 2014. |
|
Ni Miss Kipaji 2014 ;Irine Ahmed Makwaiya [20]Mrembo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kishapu |
|
MISS Redd's Shinyanga 2014 Nicole Sarakikya katikati akiwa na Mshindi wa Pili Mary Bugingo kulia kwake na Rachel Mushi ambaye ni Mshindi wa Tatu. |
|
JAJI Mkuu katika Shindano la Miss Redd's Shinyanga 2014,Frola Lauwo akitangaza matokeo. |
|
JAJI ,MKUU katika Shindano la Miss Redd's Shinyanga 2014,Flora Lauwo akimvisha taji hilo Mrembo Nicole Sarakikya. |
|
MISS Redd's Shinyanga 2014 Nicole Sarakikya na mshindi wa pili wa shindano hilo,Mary Bugingo wakikumbatiana kwa furaha mara baada ya kutangazwa kuwa ni Washindi. |
|
MFALME wa Muziki wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati,Mzee Yusuf akitoa burudani katika kinyang'anyiro cha kumpata Mnyange wa Mkoa wa Shinyanga "Miss Redd's Shinyanga 2014" |
|
HAWA ni Walimbwende walioingia tano bora katika Shindano la Miss Redd's Shinyanga 2014. |
|
WANYANGE waliobahatika kuingia Kumi bora katika Shindanno la kumsaka Miss Redd's Shinyanga 2014 wakiwa na nyuso zenye bashasha. |
HATIMAYE Mkoa wa Shinyanga
umempata mrembo atakayewakilisha Miss Redd’s Kanda ya Ziwa hivi karibuni,Mrembo
huyo aliyetwaa taji la Miss Redd’s Shinyanga 2014 ni Nicole Franklyn Sarakikya
[21] mrembo kutoka wilaya ya Kishapu.
Nicole alipata taji hilo
kwenye kinyang’anyiro kilichofanyika Juni 28,mwaka huu katika ukumbi wa Shirika
la Hifadhi ya Jamii “NSSF”wilaya ya Kahama.
Warembo wote 20 walipita
jukwaani kwa kuonyesha mavazi ya ubunifu bila kusahau burudani iliyoporomoshwa
na Mfalme wa Muziki wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati;Mzee Yusuf,Msanii Amani
kutoka Kenya,MO Music pamoja na madansa machachari kutoka Kanda ya Ziwa.
Baada ya mchakato
walitangazwa washindi walioingia Kumi bora,wakafuatiwa na tano bora wakiongozwa
na Mary Bugingo,Rachel Mushi,Neema Kakimpa,Nyangi Warioba na Nicole Sarakikya.
Majira ya Saa Nane Usiku
ndipo Jaji Flora Lauwo alimtangaza mwanadada Nicole kuwa Miss Redd’s Shinyanga2014,ukumbi
mzima ulizizima kwa shangwe huku moja ya sifa iliyomuwezesha mwanadada huyo
kutwaa taji hilo ni kujibu swali la ufahamu kwa makini zaidi akitumia lugha ya
Kiengreza.
Kwa kutwaa taji hilo
Nicole mbali ya kuuwakilisha mkoa nwa Shinyanga katika kinyang’anyiro cha Miss
Redd’s Kanda ya Ziwa pia alipata Shilingi Laki Tano sambamba na Tarakilishi
Mpakato {Laptop}yenye thamani ya Shilingi Laki Saba,huku mshindi wa pili Mary
Emmanuely Bugingo [20]kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ushetu akipata Shilingi
350,000/= na Mshindi wa tatu akiibuka Mrembo kutoka Shinyanga Vijijini;Rachel
Mushi [21] aliyepata kitita cha Shilingi 250.
Mshindi wa Nne Nyangi
Warioba [22] kutoka Halmashauri ya wilaya ya Msalala na Mshindi wa Tano Neema
Saimon Kakimpa [21] wa Kahama wote walipata kila mmoja Shilingi 150,000/= huku
walioingia Kumi bora wakipatiwa kila
mmoja Shilingi Laki Moja.
Aidha katika mchuano huo
Mrembo Irine Ahmed Makwaiya kutoka tena wilayani Kishapu aliibuka kidedea kuwa
Miss Vipaji 2014 na kujinyakulia kitita cha Shilingi Laki Tatu,baada ya
kuwashinda wenzake;Nicole Sarakikya,Jacline Jackson, na Nilam Siraji Abdul.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI