Tuesday, July 1, 2014

AVEVA RAIS WA SIMBA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


WANACHAMA wa Simba Sport Club wakiwa na shauku ya kusikiliza matokeo ya kura walizopiga.

Evans Eliaza Aveva akitoa neno la shukrani kwa wanachama baada kushinda kuwa Rais wa Simba Sport Club.


WAGOMBEA wadhifa wa Rais wa timu ya Simba;Evans Aveva mwenye suti na Andrew Tupa wakipiga kura.

Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi na aliyesimamia zoezi la uchaguzi, Amin Bakhresa,akisoma matokeo


Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi na aliyesimamia zoezi la Mkutano Mkuu, Amin Bakhresa,akimpongeza mshindi wa wadhifa wa Rais wa Simba;Evans Eliaza Aveva.
WANACHAMA wakiwa katika mstari tayari kwa kupiga kura


RAIS wa Simba Evans Aveva akiwashukuru wanachama kumchagua.

MWENYEKITI wa zamani wa Simba,Hassan Dalali akipiga kura.

 MGOMBEA Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba Sport Club;Jamhuri Kiwelo akipiga kura.
MWENYEKITI wa Simba aliyemaliza muda wake;Alhaj Ismail Aden Rage,akimpongeza Aveva.


MAKAO Makuu ya Simba Sport Club


HATIMAYE baada ya malumbano kwa zaidi ya mwezi kuhusiana na uchaguzi mkuu,wanachama wa Simba wameamua kumpa Evans Elieza Aveva dhamana ya kuwa kiongozi wa kwanza atakayetumikia wadhifa wa juu utakaotambulika kwa cheo cha Rais.

Wanachama hao waliamua kumpa dhamana hiyo Aveva,ya kuiongoza klabu hiyo ambayo inahitaji mabadiliko makubwa kutokana na kupoteza muelekeo katika soka la nchini na nje ya nchi.

Katika uchaguzi huo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,Zacharia Hanspoppe aliokoa jahazi baada ya kutoa Sh.Milioni 20 na kuwezesha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi uliomweka madarakani Aveva..

Hanspoppe alitoa fedha hizo ili kugharamia uchaguzi baada ya kampuni ya bia Tanzania (TBL), ambao ndio wadhamini wa klabu hiyo, walioahidi kugharamia mkutano huo kushindwa kufanya hivyo kwa wakati.

Habari za ndani zilidai kwamba, rais aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage alitaka uchaguzi usifanyike kutokana na wadhamini kutotoa fedha hizo;huku aliyekuwa Mgombea Urais na kisha kuenguliwa Michael Richard Wambura akikutana na kizingiti cha kuzuiwa kushiriki Uchaguzi huo kwa madai si Mwanachama.

Uchaguzi huo uliohudhuriwa na wanachama 2,501 ulifanyika kama ilivyotarajiwa huku Aveva akionekana kukosa upinzani baada ya kuibuka na ushindi wa kura  1,455 dhidi ya mpinzani wake Andrew Peter Tupa, aliyepata kura 388.

Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi na aliyesimamia zoezi hilo, Amin Bakhresa, wakati akitangaza matokeo hayo alisema kuwa mshindi wa nafasi ya Makamu wa Rais ni Geofrey Nyange ‘Kaburu’ aliyepata kura 1,046 na kuwashinda Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ (412), Swedy Mkwabi (373) na Bundala Kabula kura 25.

Bakhresa aliwataja wagombea watano waliochaguliwa kuunda Kamati ya Utendaji ni Iddi Kajuna aliyepata kura 893, Said Tully (788), Collins Frisch (758), Ally Suru ( 627) na kwa upande wa mwanamke aliyeshinda ni Jasmine Badour alyepata kura 933 na kuwashinda Asha Muhaji aliyepata kura 623 na Amina Poyo (330).

Wakati huo huo,Kamati ya Usajili iko katika hatua ya mwisho kumnasa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda, Hassan Waswa ili kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji wa timu hiyo.

Hata hivyo ilibainika baada ya uongozi mpya kuingia madarakani utafanya maamuzi ya mwisho ya kuona ni wachezaji wangapi watabaki kuichezea Simba katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayoanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu.


Aidha kwa upande wake RAIS mpya wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Evans Aveva, amesema kwamba anawaahidi wanachama wa klabu hiyo waliomchagua hatawaangusha baada ya kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi kingine cha miaka minne atakayokaa madarakani kwa mujibu wa katiba.

 Akizungumza muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika jana Jumapili kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay jijini, Aveva, alisema kuwa anafahamu kazi yake anayotakiwa kuifanya akiwa madarakani ambayo wanachama wa Simba imewaumiza kwa kipindi cha miaka minne iliyomalizika.

Aveva alisema kwamba atahakikisha anavunja makundi yaliyopo katika klabu hiyo ili kuleta umoja, ushirikiano na mshikamano ndani ya klabu hiyo na anafahamu wazi makundi hayo yalikuwepo kama sehemu ya kutekeleza demokrasia ya kila mwanachama.

Alisema kuwa makundi hayo yatakapomalizika ndipo mafanikio na maendeleo ya pamoja yatatimia na hilo ndiyo jambo ambao Wana-Simba wanatakiwa kulitekeleza kwa pamoja ili kufikia malengo waliyojiwekea.


 “Uchaguzi umemalizika na kinachotakiwa kufuata ni wanachama kujipanga kwa ajili ya kuimarisha umoja na utulivu ili mpira uchezwe ndani ya timu yetu”Alisema Aveva.

Awali akijinadi kuomba kura kwenye ukumbi huo wa uchaguzi, Aveva, alisema kuwa mara atakapofanikiwa kuingia madarakani atahakikisha anaongeza idadi ya wanachama wa klabu hiyo kutoka 7,000 na kufikia 50,000.

Aveva alisema kuwa anaamini kwa kuongeza wanachama, klabu yao itaweza kupata rasilimali watu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kujiongezea mapato na kuwataka wanachama wawe wanalipa ada zao kila mwaka na si kusubiri wakati wa uchaguzi.

Alisema anauzoefu ndani ya Simba na akiwa mwenyekiti wa kamati mbalimbali alizoziongoza aliipatia klabu mafanikio hivyo watarajie mazuri zaidi baada ya yeye kupata ridhaa ya wanachama ya kuwa rais mpya na wa kwanza wa Wekundu wa Msimbazi.


KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI