WASANII wa kucheza muziki wa kundi la Wasafi kutoka kijiji cha Kakola wakishiriki katika mchuano ulioandaliwa na Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika fainali iliyofanyika viwanja vya shule ya msingi Kakola usiku wa Alhamisi,na kufanikiwa kuwa washindi wa Pili.
MSANII wa Muziki wa kizazi kipya Mwasiti na wacheza shoo wake kutoka kundi la THT wakiwaburudisha mamia ya wakazi wa Kakola katika hafla ya utoaji wa seti ya Luninga na king'amuzi chake kwa wakazi wa Kata ya Segese,iliyotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kwenye viwanja vya shule ya Msingi Kakola ambapo pia kuna Runinga kubwa inayotumika kwa wakazi wa mji huo kutazama michuano ya Kombe la Dunia bure.
MSANII wa Muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almas "Mwasiti"sambamba na wacheza shoo wake ambao wote ni wasanii wa kundi la Tanzania House of Talent (THT).
wakitoa burudani kwa wakazi wa kijiji cha Kakola katika hafla ya utoaji wa seti ya
Luninga na king'amuzi chake kwa wakazi wa Kata ya Segese,iliyotolewa na
Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kwenye viwanja vya shule ya Msingi Kakola
ambapo pia kuna Runinga kubwa inayotumika kwa wakazi wa mji huo
kutazama michuano ya Kombe la Dunia bure.
KAMPUNI ya Africani Barrick Gold Mine kupitia
mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu umesaidia kuonekana kwa urahisi na bure kwa
michuano ya Kombe la Dunia kwa wakazi wanaoishi kuzunguka eneo la mgodi huo kwa
kusambaza seti za Luninga katika maeneo ya wazi.
African Barrick Gold Mine Ltd usiku wa mwishoni
mwa wiki iliyopita ilikabidhi seti ya Runinga kubwa na mtandao wake
kwa wananchi wa Kata ya Segese wakati wa pambano baina ya England na Colombia,hatua itakayosaidia wakazi
wa vijiji vitatu vya Segese,Bumva na Wisolele katika Kata hiyo kuangalia kombe
la dunia katika fainali zinazoendelea nchini Brazil.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Gordon
Bradley wakati akikabidhi seti hiyo na king’amzi chake alisema lengo la Kampuni
yake ni kuwafanya wananchi wakae pamoja kwa amani na utulivu katika muda wote
wa fainali za kombe la Dunia zinazoendelea na kuondoa usumbufu wa kufuata kumbi
zinazoonyesha michuano hiyo kwa ujira na zikiwa mbali na makazi.
Akizungumza awali Afisa uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu
Abdalla Msika alisema luninga hiyo ni muendelezo wa misaada mingine
inayotolewa na kampuni hiyo kwa lengo la kuimalisha mahusiano na wananchi wa
wilaya ya Kahama
Alisema katika fainali hizo za kombe la dunia
mtendaji huyo mkuu ametumia fursa ya kuangalia mechi kati ya England na
Colombia na wananchi wa kakola kwa kutumia luninga iliyofungwa kwenye shule ya
msingi kakola A lengo likiwa ni kuonyesha upendo na mshikamano wa kijamii baina
ya Mwekezaji na wananchi.
Kabla ya hapo kampuni hiyo ilitoa luninga kubwa
zingine kwa ajili ya kuangalia kombe la dunia katika miji ya Kahama, Mwendakulima,
Kakola, na sasa Segese ambapo pia wananchi wa eneo hilo wataangalia fainali
hizo bure.Na kabla ya kukabidhi seti hiyo Afisa Mtendaji huyo alitoa zawadi
mbalimbali kwa washindi wa sanaa ya kuimba na kucheza muziki.
Kwa upande wake Diwani
wa Kata ya Segese Joseph Manyala akipokea msaada wa frati skirni yenye ukubwa
wa nchi 50’’ na king’amuzi na ungo wa DSTV vyote vikiwa na thamani
ya Shilingi Milioni tatu aliomba mshikamano zaidi baina ya wananchi na mwekezaji ili kudumisha amani maeneo ya Mgodi.
Aliwataka wananchi kuendelea kuishi kwa
mahusiano mema, upendo na mshikamano na muwekezaji huyo
kampuni ya Barrick hatua itakayomhamasisha kuchangia zaidi shughuli mbalimbali
za maendeleo ya Kijamii.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI