WAREMBO walioingia kambini Ihesa Hotel &Resort ya mjini Kahama wakijifua tayari kuwania Taji la Miss Redd's Shinyanga 2014 |
WANYANGE wanaotarajia kuwania Taji la Redd's Miss Shinyanga 2014 wakiwa katika mazoezi. |
ASELA Magaka akiongea wakati wa utambulisho wa kambi ya Redd's Miss Shinyanga. |
MWAKILISHI kutoka Kampuni ya dhahabu ya Buzwagi Barrick;Salome Makamba akiwa katikati wakijadili jambo na Mwakilishi wa TBL. |
WAREMBO watakaowania taji la Redd's Miss Shinyanga wakiwa wameketi. |
KUMEKUCHA! Mkoani Shinyanga baada ya Warembo 20
kuingia kambini katika ukumbi wa Ihesa Hotel & Resort Ltd ya mjini Kahama
kujifua tayari kwa kupanda jukwaani Juni 28,mwaka huu ndani ya ukumbi wa Shirika
la hifadhi ya jamii ( NSSF) wilayani Kahama
kuwania Taji la Redd’s Miss
Shinyanga 2014.
Wakiongea katika uzinduzi
wa Kambi ya warembo hao waratibu wa
shindano hilo,Kampuni ya Asela Promotion,ilibainisha warembo waliopo kambini
wametokana na mashindano ya Urembo kutoka katika Wilaya sita za Mkoa wa
Shinyanga ambazo ni Kishapu, Kahama, Shinyanga Mjini, Msalala Shinyanga
Vijijini na Ushetu.
Mkurungezi wa Kampuni
inayoandaa shindano hilo,Asela Magaka alijinasibu kuwa mwaka huu anatarajia Redds
Miss Tanzania 2014 atatoka mkoa wa Shinyanga kutokana na warembo waliopo
kambini kuwa na vigezo,mvuto mkubwa na viwango vinavyofaa kunyakua taji hilo.
Magaka aliwataja warembo
hao kuwa ni Aisha Ally,Grace Lyimo,Pendo Maxmillian,Mary Bugingo,Irine
Hamedi,Neema Kakimpa,Jacquline Robert,Nilam Siraji,Grace Kimaro,Sophia
Mhina,Jacline Kimambo,Rose Shunda na Lawrancea Mathew.
Aliwataja Warembo wengine
kuwa ni Rachel Mushi,Hadija Nyanda,Nyangi Warioba,Rockie Bangili,Jacline
Jacksoni,Lukia Samili na Nicole Sarakikya hivyo kuwataka mashabiki na wapenzi
kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani anatwaa taji laMrembo wa Mkoa wa
Shinyanga.
Aidha aliwataja wadhamini
wa Shindano hilo kuwa ni SSCN TV ya Mjini Kahama, Nonema Investiment, Trixie
Social Media Market, Nyamizi Secretarial Service, Royal Supermarket, NSSF, Coca
Cola, Redds na Global Publisher.
Wengine ni pamoja na
Clouds FM, Three Jays’s Inverstment, CXC Africa, Williamson Diamond, Saluti,
Ihesa Hotel, Kahama Commonity Health Dispensary, Tulliz Fashion, Ngeleja Gold
Mine, Kahama Motel, Charitk Pub, Glory Pads na Barrick Buzwagi.
Mratibu huyo pia alisema kampuni
yake imejipanga kuleta wasanii mahiri watakaotoa burudani katika fainali hizo ambazo
warembo hao mbali ya kuchuana kuwania taji hilo watatoa burudani mbalimbali
ikiwemo kuonyesha vipaji vyao vya mbalimbali vya kuzaliwa.
Alisema tayari Kampuni
yake imeishaongea na Wasanii;Mfalme wa miondoko ya taarabu nchini Mzee Yusuph
na kundi la Mo Music sambamba na msanii kutoka nchini Kenya aitwae Amani kutoa
burudani katika kinyang’anyiro hicho.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI