MWENYEKITI wa CHADEMA wilaya ya Kahama;Juma Ntahimpera akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kakola Kata ya Bulyanhulu wilayani Kahama. |
MWENYEKITI wa CHADEMA wilaya ya Kahama;Juma Ntahimpera akisisitiza jambo katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kakola Kata ya Bulyanhulu.. |
EMMANUEL Mbise akiongea katika Mkutano huo wa hadhara |
UMATI wa watu uliohudhuria Mkutano wa Hadhara wakisikiliza kwa makini ujumbe uliokuwa ukitolewa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Kahama;Juma Ntahimpera. |
AFISA Usalama wa Kanda ya Ziwa Mashariki;Peter Machanga akiongea na wanakijiji cha Kakola katika Mkutano wa Hadhara. |
Moja ya Bango lililokuwa katika Mkutano huo wa hadhara.
BAADHI ya Umati wa wanakijiji cha Kakola waliodhuria Mkutano huo wa Hadhara. |
MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya African Gold Mine LTD
huenda ukavamiwa baada ya siku 30 na wanakijiji wanaoishi kuuzunguka iwapo madai
ya kutengewa kwa eneo la wachimbaji wadogowadogo likiendelea kupuuzwa.
Katika risala iliyosomwa na Diwani wa Kata ya
Bulyanhulu Joseph Makoba kwa niaba ya wananchi, ilidai wamechoka na umaskini
unaotokana na kupoteza muda mwingi katika kufuatilia haki yao hiyo kwa kipindi
kirefu ikiwemo kesi mbalimbali dhidi ya Mgodi huo tangu mwaka 1999,juu ya madai
yao ya fidia pasipo kutambua hatima ya hukumu zake.
Makoba alisema jamii hiyo ambayo awali iliishi kwa kutegemea uchimbaji na kulazimika kumpisha Mwekezaji imekuwa ikiishi maisha ya dhiki kutokana na kutopatiwa eneo mbadala la uchimbaji hali ambayo imesababisha baadhi yao ndoa zao kusambaratika kutokana na kuathirika kimapato hasa kwakuwa wakazi wengi pato lao linatokana na shughuli za madini.
Aidha alisema wanakijiji hao hawatasita kuvamia eneo la mgodi iwapo madai yao kuhusiana na Mwekezaji huyo kutotoa fursa ya kufanya biashara mgodini hapo japokuwa wanazalisha bidhaa bora,yasipofanyiwa mabadiriko ndani ya mwezi mmoja.
Kwa upande Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kahama Juma Ntahimpera alisema ni budi wana vijiji wanaoishi kuzunguka migodi hiyo stahiki zao wapatiwe ikiwemo kesi ya wafanyakazi na mgodi za mwaka 2004 na 2007 hukumu zake zitoke pia wachimbaji wadogo wapatiwe maeneo ili wajikimu kimaisha sambamba na mji wa Kakola kupimwa.
Alisema pamoja na Rais Kikwete kuidhinisha Kakola kutohamishwa na kutakiwa kupimwa viwanja lakini pamoja na jamii kuchangia gharama za upimaji hakuna kilichofanyika hivyo kuomba fedha za wananchi zirejeshwe na kufanya maendeleo mengine.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu,Johnson Mwakatage akiongea kwa simu na gazeti hili alidai jukumu la
kutenga maeneo ya wachimbaji wadogo ni la serikali na halina mahusiano na
Mwekezaji hivyo hatua hizo zitakuwa ni za kuhukumu mgodi ambao hauhusiki.