WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Nchini;Dk.Shukuru Kawambwa. |
HALMASHAURI
ya wilaya ya Ushetu imepata walimu wapya 275 watakaofundisha shule
mbalimbali za msingi na sekondari hali itakayopunguza tatizo la upungufu wa
walimu katika Halmashauri hiyo.
Hali
hiyo ilielezwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo;Isabela Chilumba,ambapo alisema kati ya hao 75 ni
wenye Shahada ya kwanza huku 33 wakiwa na elimu ya Stashahada.
Aidha
Chilumba alisema walimu hao watapangwa katika Shule za Sekondari kumi na sita
ikiwemo moja ya Dakama inayotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa na kidato cha sita,katika mgawo huo kila shule itapata wastani
wa walimu sita hadi saba.
Hata
hivyo Chilumba alisema kwa upande wa Shule za Msingi, Halmashauri yake imepata walimu
167 ambao watasambazwa kwenye maeneo yenye upungufu wa walimu ili kuondoa
kabisa tatizo hilo
kwenye shule zake za Msingi.
Pamoja
na idadi hiyo;Chilumba alisema kwa utaratibu huo ifikapo mwaka kesho kama Halmashauri
yake itapata idadi ya walimu kama hiyo tatizo
la upungufu wa walimu litakuwa limemalizika kabisa na kuinua kiwango cha elimu.
Mkurugenzi
huyo aliipongeza serikali kwa jitihada zake za kumaliza tatizo la upungufu wa
walimu kwenye shule zikiwemo sekondari za Kata ambazo baadhi ya jamii wamekuwa
wakizibeza wakiziita yeboyebo huku baadhi yake mwaka huu zikiwa zimefanya vizuri
katika mitihani ya kidato cha nne.
Wilaya
ya Kahama ina Halmashauri tatu za Ushetu,Mji na Msalala huku Ushetu ikiongozwa
kwa ukubwa wa eneo na idadi ya watu hali ambayo Mkurugenzi huyo alidai ni
changamoto za kiutendaji anazokumbana nazo.